Michezo

Ratiba ya michuano ya ligi ya Super 8

September 8th, 2018 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

Huku zikiwa zimebakia katika mechi saba za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Super 8, michuano hiyo inaingia wiki yake ya 24  Jumapili kwa mechi kadhaa katika viwanja mbali mbali.

Ni pointi tano zinatenganisha timu za Jericho All Stars (pointi 49) na Makadara Junior (44), TUK (42), NYSA (38), Kawangware United (37) na Meltah Kabiria (35) ambazo zote zina nafasi ya kutwaa ubingwa.

Jericho All-Stars ambao majuzi watoka sare  1-1 na MASA wamo kileleni kwa tofauti ya pointi tano kwenye ligi hiyo inayojumuisha timu 16 baada ya kushinda mara 14 na droo saba.

Ratiba ya mechi za kesho ni: 

Zamalek na Kawangware United (Drive Inn grounds- saa tisa)

Kayole Asubuhi na Meltah Kabiria (Calvary grounds- saa kumi),

Jericho All Stars na Metro Sports (Camp Toyoyo- saa tisa),

Makadara Junior League SC na RYSA (Camp Toyoyo- saa tano),

Rongai All Stars na Shauri Moyo Blue Stars (Nakeel grounds- saa tisa),

NYSA na Shauri Moyo Sportiff (Ngong Posta- saa tisa),

Team Umeme na MASA (Ziwani grounds- saa kumi),

TUK na Leads United (Kabete Campus- saa tisa).