Michezo

Ratiba ya SportPesa Shield

March 29th, 2019 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

VITA vya kuwania tiketi ya kuwakilisha Kenya katika soka ya Kombe la Mashirikisho la Afrika msimu 2019-2020 vitapamba moto wikendi hii wakati Kombe la Ngao litaingia raundi ya 16-bora.

Washindi wa makala mawili yaliyopita Kariobangi Sharks (2018) na AFC Leopards (2017) watateremka uwanjani kuzichapa dhidi ya Murang’a Seal na Bungoma Superstars mnamo Machi 31 na Aprili 1, mtawalia.

Sharks na mabingwa mara nane Leopards walikuwa na mtihani rahisi katika mechi zao za raundi ya 32-bora walipopeta Elim 5-0 na Transfoc 4-0 mnamo Machi 16 uwanjani Bukhungu, mtawalia. Seal ilijikatia tiketi kwa kunyuka Kisumu All Stars 4-1 nayo Bungoma Superstars ikashangaza japo kwa njia ya penalti 5-4 mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 2009 Sofapaka, ambao walishinda Kombe la Ngao mwaka 2007, 2010 na 2014.

SS Assad kutoka Pwani, ambayo pia iliduwaza klabu ya Ulinzi Stars kutoka Ligi Kuu kwa penalti 5-4, itaingia uwanjani Jumamosi kuvaana na Naivas.

Washikilizi wa rekodi ya mataji mengi ya Kombe la Ngao, Gor Mahia watamenyana na washindi wa mwaka 2015 Bandari mnamo Aprili 10.

Washindi wa kombe hili la muondoano watatuzwa Sh2 milioni pamoja na kunyakua tiketi ya kushiriki Kombe la Mashirikisho, ambalo ni la daraja ya pili barani Afrika.

RATIBA (16-BORA)

Machi 30

Mwatate United na Congo Boys (Wundanyi, 3.00pm)

SS Assad na Naivas (Ukunda, 3.00pm)

Bidco United na Dero FC (Thika, 3.00pm)

KCB na Vihiga Sportiff (Machakos, 3.00pm)

Machi 31

Western Stima na Wazito (Moi Kisumu, 4.00pm)

AFC Leopards na Bungoma Superstars (Bukhungu, 4.00pm)

Aprili 1

Kariobangi Sharks na Murang’a Seal (Kasarani, 4.00pm)

Aprili 10

Bandari na Gor Mahia (Mbaraki, 4.00pm)

MATOKEO YA RAUNDI YA 32-BORA:

Uprising 0-5 Western Stima (Ruaraka)

Congo Boys 2(3)-2(2) Kenya Police (Serani)

SS Assad 0(5)-0(4) Ulinzi Stars (Ukunda)

Bungoma Superstars 0(5)-0(4) Sofapaka (Sudi)

Murang’a Seal 4-1 Kisumu All Stars (Kiharu)

Transmara Sugar 0-1 Bidco United (Gusii)

Dero 2-0 FC Talanta (Moi Kisumu)

Sindo United 0-1 KCB (Moi Kisumu)

Vihiga Sportif 2-0 Ushuru (Mumias)

Elim 0-5 Kariobangi Sharks (Bukhungu)

Transfoc 0-4 AFC Leopards (Bukhungu)

Kayo 0-1 Bandari (Ruaraka)

Fortune Sacco 0-1 Wazito (Thika)

Emmausians 0-6 Mwatate United (Serani)

Naivas 0-1 Equity (Camp Toyoyo)

Kenpoly 0-4 Gor Mahia (Machakos)