RB Leipzig wachabanga Werder Bremen na kutinga fainali ya German Cup

RB Leipzig wachabanga Werder Bremen na kutinga fainali ya German Cup

Na MASHIRIKA

FOWADI Emil Forsberg alitokea benchi na kufunga bao la dakika za mwisho lililowazolea RB Leipzig ushindi wa 2-1 dhidi ya Werder Bremen mnamo Aprili 30, 2021.

Ushindi huo wa Leipzig uliwawezesha kufuzu kwa fainali ya German Cup. Forsberg aliwafungia Leipzig bao la ushindi katika dakika ya 121 na baada ya vikosi vyote viwili kufungana katika muda wa kawaida wa dakika 90.

Hwang Hee-chan aliwaweka Leipzig kifua mbele katika dakika ya 93 kabla ya Bremen kusawazishiwa na Leonardo Bittencourt mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha muda wa ziada.

Borussia Dortmund watapepetana na Holstein Kiel ya Ligi ya Daraja la Pili kwenye nusu-fainali ya pili ya German Cup.

Ushindi wa Leipzig unamaanisha kwamba kocha Julian Nagelsmann ana fursa ya kuongoza waajiri wake kunyanyua taji la kwanza la haiba kubwa katika historia yao kwenye mapambano ya haiba kubwa kabla ya kuyoyomea Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitano kuanzia mwisho wa msimu huu wa 2020-21.

Kocha raia wa Amerika, Jesse Marsch wa Red Bull Salzburg ndiye anayetarajiwa kujaza pengp la Nagelsmann kambini mwa Leipzig mwishoni mwa muhula huu.

Fainali ya German Cup msimu huu imeratibiwa kusakatwa mnamo Alhamisi ya Mei 13, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Cavani kurefusha mkataba Man-United

Uingereza wapewa Ireland ya Kaskazini kwenye mchujo wa...