Re-Union FC yaweka mikakati kurejesha fahari kama zamani

Re-Union FC yaweka mikakati kurejesha fahari kama zamani

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wa Re-Union FC, Moses Were amesema kuwa wamepania kupigana kwa udi na uvumba kwenye Ligi ya Kaunti, FKF, Nairobi West kuwania tiketi ya kufuzu kupandishwa ngazi kushiriki Ligi ya Kanda hiyo muhula huu.

Anashikilia kuwa wanahitaji kurejea kucheza michuano ya hadhi ya juu nchini.

”Tunalenga kujitahidi kiume kuhakikisha tumerejea kushiriki kampeni za Ligi Kuu nchini miaka ijayo,” alisema na kuongeza kuwa wanapaswa kuwa wakishiriki ligi moja na waliokuwa mahasimu wao Gor Mahia na AFC Leopards.

Alisema kuwa klabu hiyo ilishushwa ngazi na kudidimia baada ya kukosa ufadhili kugharamia shughuli za michezo.

Anadokeza kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri ambao wakipigwa jeki wana uwezo tosha kufanya vizuri na kutimiza malengo kwenye mchezo huo.

Kwenye matokeo ya mechi za wikendi, Re-Union ilizamisha Usaclife FC ya Eastleigh kwa mabao 2-1 ugani Umeme Ziwani, Nairobi. Re-Union ilipata mbao hayo kipindi cha kwanza kupitia juhudi zake Seth ‘Kasisi’ Omondi na Dickson Gitahi. Usaclife FC ilipata bao la kufuta machozi dakika ya 72 lililotupiwa wavuni na Samson Otieno.

  • Tags

You can share this post!

Otieno afungia AIK bao kuibuka mchezaji bora wa mechi Uswidi

UFUGAJI: Anazingatia mbinu bora kuwafuga ng’ombe wake

T L