Michezo

Real Madrid wanyanyua taji la 15 la Klabu Bingwa Ulaya

June 2nd, 2024 1 min read

NA REUTERS

REAL Madrid wamepiga Borussia Dortmund 2-0 kunyanyua taji la 15 la Klabu Bingwa Ulaya na kuendeleza ubabe katika historia ya Uefa.

Dani Carvajal na Vinicius Junior ndio waliotia kimiani mabao hayo.

Fainali ilisakatwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Wembley jijini London, Uingereza.