Real Madrid wazamisha Valencia na kukaribia tena Barcelona kileleni mwa jedwali la La Liga

Real Madrid wazamisha Valencia na kukaribia tena Barcelona kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

REAL Madrid walifunga mabao mawili ya haraka mwanzoni mwa kipindi cha pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Valencia mnamo Alhamisi na kupunguza pengo la alama kati yao na Barcelona wanaoselelea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

Matokeo hayo yalidumisha Real katika nafasi ya pili jedwalini kwa alama 45, tano nyuma ya Barcelona ambao pia wametandaza mechi 19.

Real waliwekwa kifua mbele na Marco Asensio katika dakika ya 52 kabla ya Vinicius Jr aliyekuwa akichezea Real mara ya 200 kucheka na nyavu za Valencia dakika mbili baadaye.

Gabriel Paulista wa Valencia alionyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 72 kwa kosa la kumchezea Vinicius visivyo.

Bao la Antonio Rudiger aliyejaza kimiani krosi ya Luka Modric mwishoni mwa kipindi cha kwanza lilifutiliwa mbali baada ya teknolojia ya VAR kubainisha kwamba tayari Karim Benzema alikuwa amemchezea visivyo Yunus Musah ndani ya kijisanduku.

Fowadi mzoefu raia wa Ufaransa, Benzema, 35, aliondolewa uwanjani akichechemea huku akiashiria kupata jeraha la paja. Real watakuwa wageni wa Liverpool kwa ajili ya mchuano wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Februari 21 na huenda Benzema akanogesha mchuano huo.

Hata hivyo, kocha Carlo Ancelotti amefichua mpango wa Real kuwania huduma za fowadi Gabriel Jesus wa Arsenal ili ajaze nafasi ya Benzema mwishoni mwa msimu huu wa 2022-23.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wanahabari wapinga kuzuiwa kuingia bunge

CECIL ODONGO: Kinaya Kenya kupatanisha mataifa mengine...

T L