Real Madrid yacharaza Sevilla na kufungua mwanya wa pointi nne kileleni mwa jedwali la La Liga

Real Madrid yacharaza Sevilla na kufungua mwanya wa pointi nne kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

VINICIUS Junior alifunga bao mwishoni mwa kipindi cha pili na kusaidia Real Madrid kutoka nyuma na kupepeta Sevilla 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) iliyochezewa ugani Bernabeu mnamo Jumapili usiku.

Alama tatu ambazo Real walijizolea katika mechi hiyo ziliwawezesha kufungua mwanya wa pointi nne kileleni mwa jedwali la La Liga.

Rafa Mir aliwaweka Sevilla kifua mbele katika dakika ya 12 kabla ya Karim Benzema kusawazisha mambo dakika 20 baadaye. Vinicius alijaza kimiani bao lililowapa Real ushindi katika dakika ya 87.

Hiyo ilikuwa mechi ya sita mfululizo kwa Real ya kocha Carlo Ancelotti kushinda katika mashindano yote ya muhula huu. Kikosi hicho kwa sasa kinaselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 33, nne zaidi kuliko mabingwa watetezi Atletico Madrid waliokomoa Cadiz 4-1 kupitia mabao ya Thomas Lemar, Antoine Griezmann, Angel Correa na Matheus Cunha.

Nambari tatu Real Sociedad pia wanajivunia alama 29, moja zaidi kuliko Sevilla wanaofunga mduara wa nne-bora.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Okumu arejea kikosini Gent ligini Ubelgiji, Kapaito aokoa...

WANYONYI CUP: Red Carpet, Uthiru, WYSA zasonga mbele...

T L