Michezo

Real Madrid yashtaki refarii kupuuza visa vya kiubaguzi dhidi yao

March 21st, 2024 2 min read

NA MASHIRIKA

MADRID, Uingereza

KLABU ya Real Madrid imewasilisha kesi dhidi ya refarii aliyechezesha mechi kati yao na Osasuna, ikidai hakuandika kwenye ripoti yake vitendo vya kiubaguzi alivyofanyiwa mshambuliaji Vinicius Junior.

Tungependa kusema hapa wazi kwamba refarii Juan Martinez Munuera alipuuza matusi na foka zilizoelekezwa kwa Vinicius Junior, mwishoni mwa wiki.

Osasuna wamekanusha madai kwamba mashabiki wao walimfokea kwa matusi ya kikabila straika huyo ambaye amekuwa nchini Uhispania kwa miaka mitatu iliyopita.

Lakini Real Madrid inataka hatua ichukuliwe ili kumaliza tabia hiyo baada ya mchezaji huyo kufanyiwa hivyo mara kwa mara.

Baada ya kushutumu vikali ripoti hiyo, vile vile klabu ya Madrid imewasilisha ripoti hiyo kwa kamati ya kiufundi ya Shirikisho la Soka Uhispania.

Vinicius ambaye ni raia wa Brazil aliye na umri wa miaka 23, alifunga mabao mawili katika ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Osasuna ugani El Sadar, matokeo ambayo yameifanya Madrid kuongoza msimamo wa La Liga kwa pengo la pointi 10.

Awali, Real Madrid iliwasilisha kesi nyingine mbili baada mchezaji huyo kufanyiwa vitendo kama hivyo na mashabiki wa timu za Atletico Madrid na FC Barcelona.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Brazil amekuwa akirushiwa matusi ya kiubaguzi mara kwa mara katika misimu kadhaa iliyopita.

Mechi hizo ni pamoja na ile iliyokutanisha Atletico Madrid na Real Madrid iliyochezwa Septemba 2022 ugenini nje ya uwanja na kabla ya mechi kuanza.

Mnamo Juni 2023, mashabiki wanne walipigwa faini ya Sh8.7 milioni na kupigwa marufuku miaka miwili kuingia uwanjani baada ya kupatikana na hatia ya kumrushia matusi staa huyo karibu na mahali Real Madrid wanafanyia mazoezi.

Wengine watatu walipigwa faini Sh800 milioni na kupigwa marufuku ya mwaka mmoja kwa kutoa matusi ya kiubaguzi mwezi mwaka uliopita Mei katika mechi kati ya Madrid na Valencia.

Msimu huu kumekuwa na ripoti za matusi ya kiubaguzi dhidi ya Vinicius wakati Madrid wakicheza na Sevilla mwezi Oktoba, dhidi ya Barcelona siku chache baadaye na dhidi ya Valencia mwezi huu.