Real Sociedad watua kileleni mwa jedwali la Liga baada ya kutoka sare na Atletico

Real Sociedad watua kileleni mwa jedwali la Liga baada ya kutoka sare na Atletico

Na MASHIRIKA

REAL Sociedad walirejea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) licha ya mabao mawili waliyofungwa na fowadi Luis Suarez wa Atletico ambao ni mabingwa watetezi kuwanyima ushindi.

Sociedad walioshinda taji la La Liga kwa mara ya mwisho mnamo 1982, walijipatia uongozi wa 2-0 baada ya Alexander Isak kushirikiana na Alexander Sorloth. Hata Hivyo, Suarez ambaye ni mwanasoka wa zamani wa Liverpool na Barcelona aliwarejesha Atletico mchezoni kupitia mpira wa kichwa aliopokezwa na Joao Felix.

Fowadi huyo veterani alisawazishia Atletico kupitia penalti na kufanya mambo kuwa 2-2 baada ya kuchezewa visivyo na Mikel Merino. Sociedad kwa sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la La Liga kwa alama 21, moja zaidi kuliko Sevilla na Real Madrid waliopepeta Barcelona 2-1.

Nambari tatu Sevilla walikomoa Levante 5-3 katika mchuano mwingine huku Atletico wakishikilia sasa nafasi ya nne kwa alama tatu nyuma ya viongozi.

You can share this post!

Mung’aro alitiliwa sumu, wandani wadai

WANDERI KAMAU: Mataifa yazingatie uhuru wa kila mtu...

T L