Redio za lugha mama zatakiwa ziwe na vipindi kuhusu jamii

Redio za lugha mama zatakiwa ziwe na vipindi kuhusu jamii

NA KENYA NEWS AGENCY

KATIBU katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia (ICT) Esther Koimett amezitaka redio zinazotangaza kwa lugha ya mama kukumbatia vipindi ambavyo vitasaidia kuimarisha jamii kimaendeleo.

Bi Koimett alisema vipindi hivyo vinafaa kujikita katika elimu, kilimo na biashara kwa sababu ni kati ya masuala ambayo yatasaidia kuhamasisha jamii kujijenga kiuchumi.

Alikuwa akizungumza kwenye eneobunge la Eldama Ravine wakati wa kuzindua redio mpya ya Wingu.

Aliongeza kuwa wizara yake inashirikiana na Baraza la Vyombo vya Habari kuibuka na mwongozo wa kuwapa wanahabari mafunzo ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufuata sheria za taaluma yao.

  • Tags

You can share this post!

JKF yatenga Sh22.2 milioni kwa wanafunzi kutoka familia za...

TAHARIRI: Viongozi waache kuingiza siasa katika mambo...

T L