Michezo

Refarii wa Kombe la Dunia afunga mkewe bao la mapenzi

January 20th, 2024 1 min read

NA CHRIS ADUNGO

REFARII raia wa Argentina, Nestor Pitana, aliyepuliza kipenga kwenye fainali ya Kombe la Dunia iliyokutanisha Ufaransa na Croatia nchini Urusi mnamo 2018, anatarajia kuwa baba mzazi baada ya mkewe, Romina Ortega, kuanza kuhudhuria kliniki.

Pitana, 48, alianza kutoka kimapenzi na Romina – ambaye ni kahaba wa zamani – mnamo 2014 baada ya kukamilika kwa Kombe la Dunia nchini Brazil.

Maamuzi ya Pitana uwanjani yalipendeza mashabiki wengi na akawa kivutio cha warembo. Hata hivyo, kidosho aliyemzingua zaidi ni Romina — mwanamitindo na mama wa watoto wawili ambaye kwa wakati huo alikuwa akiuza picha na video za uchi kupitia jukwaa la ‘OnlyFans’ mitandaoni.

“Tulifunga pingu za maisha na sasa tunatarajia kimalaika mwishoni mwa Machi,” akasema Romina kwa kufichua kuwa anatazamia kufyatua kimalaika cha kiume.

Pitana sasa ni refa wa ligi mbalimbali za Amerika Kusini. Hakuwa sehemu ya waamuzi wa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Aidha, alisema anapanga kuacha kabisa masuala ya uanamitindo ili kumakinikia familia na maisha ya ndoa na uzazi.

Pitana ambaye sasa ni refa wa ligi mbalimbali za Amerika Kusini, hakuwa sehemu ya waamuzi wa fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

“Wiki za ujauzito zimesonga sana. Zilizosalia ni za kuhesabika tu,”akaandika Romina kwenye Instagram wiki hii chini ya picha ambayo alipigwa akiwa ameshikwa tumboni na Pitana.