Michezo

RIADHA ZA MABARA: Wanariadha waliochaguliwa ni wale weledi, asema Yego

September 7th, 2018 2 min read

Na Geoffrey Anene

“YouTube man” Julius Yego anaamini wanariadha waliochaguliwa kupeperusha bendera ya Bara Afrika kwenye Riadha za Mabara (Intercontinental Cup) ndio weledi. 

Akizungumza katika kikao na wanahabari Ijumaa kabla ya mashindano haya kuandaliwa mjini Ostrava katika Jamhuri ya Czech hapo Septemba 8-9, 2018, Mkenya huyu amesema, “Nadhani tuna kikosi ambacho ni kizuri zaidi barani Afrika. Nasubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi mashindano yatakavyokuwa.”

Mbali na bingwa huyu wa zamani wa kurusha mkuki wa Afrika na Dunia, timu ya Afrika ina nyota Wakenya Emmanuel Korir (mita 800), Elijah Manangoi na Winnie Chebet (mita 1500), Edward Zakayo na Hellen Obiri (mita 3000), Conseslus Kipruto na Beatrice Chepkoech (mita 3000 kuruka viunzi na maji) na Mathew Sawe (Kuruka Juu).

Mashindano haya ya mabara yanaleta pamoja timu ya Bara Afrika, Bara Ulaya, Americas na Asia-Pacific. Washiriki wanaounda timu hizi hutolewa katika mashindano ya mabara husika kwa mfano timu ya Afrika ilipatikana baada ya Riadha za Afrika mjini Asaba nchini Nigeria zilizofanyika Agosti 1-5, 2018. Kila bara liliandaa mashindano yake na kuunda timu moja.

Timu ya Bara Afrika hii hapa chini:

WANAUME

100m: Arthur Cisse (Ivory Coast), Akani Simbine (Afrika Kusini)

200m: Baboloki Thebe (Botswana), Ncincihli Titi (Afrika Kusini)

400m: Thapelo Phora (Afrika Kusini), Baboloki Thebe (Botswana)

800m: Nijel Amos (Botswana), Emmanuel Korir (Kenya)

1500m: Elijah Manangoi (Kenya), Ronald Musagala (Uganda)

3000m: Getaneh Molla (Ethiopia), Edward Zakayo (Kenya)

3000m steeplechase: Soufiane El Bakkali (Morocco), Conseslus Kipruto (Kenya)

110m kuruka viunzi: Oyeniyi Abejoye (Nigeria), Antonio Alkana (Afrika Kusini)

400m kuruka viunzi: Cornel Fredericks (Afrika Kusini), Abdelmalik Lahoulou (Algeria)

Kuruka Juu: Chris Moleya (Afrika Kusini), Mathew Sawe (Kenya)

Kuruka kwa ufito: Mohamed Amin Romdhana (Tunisia), Valco van Wyk (Afrika Kusini)

Kuruka Umbali: Yahya Berrabah (Morocco), Ruswahl Samaai (Afrika Kusini)

Kuruka hatua tatu: Godfrey Mokoena (Afrika Kusini), Hugues Fabrice Zango (Burkina Faso)

Kurusha tufe: Chukwuebuka Enekwechi (Nigeria), Mohamed Hamza (Misri)

Kurusha kisahani: Victor Hogan (Afrika Kusini), Elbachir Mbarki (Morocco)

Hammer: Mostafa Al Gamal (Misri), Tshepang Makhethe (Afrika Kusini)

Kurusha mkuki: Phil-Mar van Rensburg (Afrika Kusini), Julius Yego (Kenya)

4x100m: Henrico Bruintjies (Afrika Kusini), Arthur Cisse (Ivory Coast), Emile Erasmus (Afrika Kusini), Simon Magakwe (Afrika Kusini), Akani Simbine (Afrika Kusini), Ncincihli Titi (Afrika Kusini)

4x400m (mseto): Nijel Amos (Botswana), Thapelo Phora (Afrika Kusini), Baboloki Thebe (Botswana)

Wakiambiaji wa ziada: Larbi Bourrada (Algeria), Ayanleh Souleiman (Djibouti)

WANAWAKE

100m: Janet Amponsah (Ghana), Marie-Josee Ta Lou (Ivory Coast)

200m: Germaine Abessolo Bivina (Cameroon), Marie-Josee Ta Lou (Ivory Coast)

400m: Christine Botlogetswe (Botswana), Caster Semenya (Afrika Kusini)

800m: Besu Sado Deko (Ethiopia), Caster Semenya (Afrika Kusini)

1500m: Rababe Arafi (Morocco), Winnie Chebet (Kenya)

3000m: Hellen Obiri (Kenya), Senbere Teferi (Ethiopia)

3000m kuruka viunzi na maji: Weynshet Ansa (Ethiopia), Beatrice Chepkoech (Kenya)

100m hurdles: Tobi Amusan (Nigeria), Marthe Koala (Burkina Faso)

400m kuruka viunzi: Lamiae Lhabz (Morocco), Wenda Nel (Afrika Kusini)

Kuruka Juu: Hoda Hagras (Misri), Erika Nonhlanhla Seyama (Swaziland)

Kuruka Umbali: Ese Brume (Nigeria), Marthe Koala (Burkina Faso)

Kuruka kwa ufito: Dina Ahmed Al-Tabaa (Misri), Dorra Mahfoudhi (Tunisia)

Kuruka hatua tatu: Grace Anigbata (Nigeria), Zinzi Chambangu (Afrika Kusini)

Kurusha tufe: Jessica Da Silva Inchude (Guinea Bissau), Ischke Senekal (Afrika Kusini)

Kurusha kisahani: Onyekwere Chioma (Nigeria), Ischke Senekal (Afrika Kusini)

Hammer: Ogunrinde Temilola (Nigeria), Soukaina Zakkour (Morocco)

Kurusha mkuki: Kelechi Nwanaga (Nigeria), Jo-Ane van Dyk (Afrika Kusini)

4x100m: Janet Amponsah (Ghana), Tobi Amusan (Nigeria), Rosemary Chukwuma (Nigeria), Blessing Okagbare (Nigeria), Marie-Josee Ta Lou (Ivory Coast), Joy Uba-Gabriel (Nigeria)

4x400m (mseto): Christine Botlogetswe (Botswana), Glory Nathaniel (Nigeria), Caster Semenya (Afrika Kusini)

Wakimbiaji wa ziada: Mercy Nti-Obong (Nigeria), Chidi Okezie (Nigeria), Besu Sado (Ethiopia), Ajayi Yinca (Nigeria)