Rift Valley Prisons yalenga kubeba taji la voliboli nchini licha ya upinzani mkali

Rift Valley Prisons yalenga kubeba taji la voliboli nchini licha ya upinzani mkali

Na JOHN KIMWERE

KIKOSI cha Maafande wa Rift Valley Prisons ni kati ya timu zinazoshiriki voliboli ya kuwania taji la Ligi Kuu ya wanaume muhula huu.

Aidha ni miongoni mwa vikosi vinavyolenga kujituma kwa udi na uvumba kwenye jitihada za kuhakikisha inamaliza kati ya nafasi bora kwenye kampeni za msimu huu. Imeorodheshwa kati ya timu nyingi tu katika idara ya Magereza zinazoshiriki voliboli ya Ligi Kuu muhula.

Kocha wake mkuu, Japheth Mwok, anasema: ”Katika mpango mzima tunalenga kukaza buti ambapo kwa mara ya kwanza tunalenga kubeba taji la msimu huu lakini tunakabiliwa na ushindani mkali.”

Anasisitiza kuwa hakuna hasiyependa kufanya vizuri lakini juhudi zao kupigania taji hilo hazijafaulu lakini wanaamani ipo siku watafanya kweli.

Kocha Japheth Mwok akiwapa wachezaji wake mawaidha wakati wa mechi ligi. PICHA | JOHN KIMWERE

Kocha huyo anashikilia kuwa wanahitaji kukaza buti mazoezini maana wapinzani wao ni timu za vikosi vya usalama katika idara za Kenya. ”Ninaamini tukimakinika zaidi katika mazoezi yetu tuna uwezo wa kukabili wapinzani wetu kiume na kumaliza katika nafasi bora,” akasema. Kikosi hicho kinajipatia miaka mitatu au minne kuhakikisha kimeibuka kati ya nafasi mbili bora na kujikatia tiketi ya kushiriki fainali za Klabu Bingwa Afrika (CAVB).

Western Prisons ambayo hufanyia mazoezi katika uwanja wa Magereza ya Kakamega ilianzishwa mwaka 1992 ili kuhakikisha maafande hao wamepata namna ya kupumzisha akili zao baada ya kazi ya siku nyingi.

Wachezaji wa Western Prisons wakicheza dhidi ya wenzao wa Mombasa Prisons. PICHA | JOHN KIMWERE

Kocha wenzake, Lambert Mayende anatoa wito kwa Shirikisho la Voliboli Nchini (KVF) kushirikiana na serikali kuhakikisha imejenga kumbi za ndani za kisasa za mchezo huo. ”Uhaba wa kumbi za ndani kwa ndani kwa kiasi fulani unadidimiza kiwango cha voliboli ya Kenya,” akasema.

Anasema mwaka 2016 ndio waliwahi kumaliza katika nafasi nzuri kwenye kampeni za kipute hicho ambapo mwaka huu wanataka kufanya bora zaidi. Hata hivyo anasema kuwa wanakabiliwa na ushindani mkali mbele ya wafalme wa mchezo huo Kenya Genaral Service Unit(GSU).

Pia Kenya Prisons, Jeshi la Ulinzi (KDF), Equity Bank na Halmashauri ya Bandari ya Kenya (KPA) kati ya zingine. Anashikilia kuwa vikosi hivyo vimekaa vizuri kuzima ndoto yao kumaliza kati ya nafasi bora msimu huu.

Anadokeza kuwa ingawa kikosi chake hakijapata mashiko vizuri, ana uwezo wa kukuza wachezaji na kufanikiwa kuteuliwa kushiriki voliboli ya kulipwa miaka ijayo.

Western Prisons inashirikisha wachezaji kama: Luke Sidi, David Tungu, Felix Omondi, Yusuf Nganyi, Jared Okweno, David Chemoges, Ladock Kipkosgei, Wisley Bitok, Ivan Mogere, Kelvin Mulinya, Jackson Kipkoech na Naman Chilongo kati ya wengine. Pai kocha huyo hushirikiana na manaibu wengine wawili akiwa Josp Barasa na Pius Mabonga.

 

  • Tags

You can share this post!

Wafuasi wa Ruto wahofia wimbi la Karua

Kiungo Danny Drinkwater aomba msamaha kwa...

T L