Habari za Kitaifa

Riggy G aondoka nchini kumwakilisha Ruto Afrika Kusini


NAIBU Rais Rigathi Gachagua anaondoka nchini Jumanne usiku kuelekea Pretoria, Afrika Kusini, siku moja baada ya Rais William Ruto kurejea nchini kutoka ziara nchini Italy na Uswizi.

Bw Gachagua anahudhuria kuapishwa kwa Rais Cyril Ramaphosa kufuatia uchaguzi uliopelekea kuundwa kwa serikali ya muungano baina ya ANC na chama kikuu cha Upinzani, DA.

Naibu Rais anamwakilisha Rais Ruto kwenye hafla hiyo ya Jumatano ambayo uchaguzi wake umeacha vyama vilivyoshindwa, vikiongozwa na rais wa zamani Jacob Zuma, vikinung’unika na kuitisha kura kurudiwa.

“Bw Gachagua atawasilisha ujumbe wa heko wa Rais Ruto kwa Rais Ramaphosa na raia wa Afrika Kusini kwa jumla,” ikasema taarifa ya Mkuu wa Mawasiliano katika Afisi ya Naibu Rais, Bi Njeri Rugene.