Ripoti yaanika jinsi makocha hutekeleza dhuluma za kimapenzi

Ripoti yaanika jinsi makocha hutekeleza dhuluma za kimapenzi

Na SIAGO CECE

MAKOCHA na mameneja wa timu za  michezo nchini hutumia vyeo vyao kuendeleza dhuluma za kijinsia na kimapenzi dhidi ya wanamichezo.

Ripoti ya uchunguzi iliyozinduliwa Jumatatu katika kongamano linaloendelea Diani, Kaunti ya Kwale, inaonyesha tabia hiyo mbaya imekithiri kwenye sekta hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jinsia na Usawa katika Michezo, Catherine Ndereba, ambaye alikuwa mwanariadha alitoa hotuba yake kwa machozi huku akisema jinsi suala la dhuluma za kijinsia linaathiri wanaspoti, hasa wanawake.

“Nilisikitika sana nilipokuwa nikifanya utafiti huu na kusikiza jinsi wanawake wanadhulumiwa. Inasikitisha zaidi kuwa hakuna haki yoyote inayotendwa ama ripoti yoyote ya washukiwa kutiwa mbaroni. Hii inafaa kubadilika,” akasema Bi Ndereba.

Waziri wa Michezo, Amina Mohammed, alisema kongamano hilo linalenga kupata suluhisho kwa changamoto wanazopitia wanawake na wanaume katika sekta ya michezo.

Bingwa wa Dunia na Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika marathon Eliud Kipchoge, alisema utovu wa nidhamu miongoni mwa wanariadha wengi huchangia dhuluma hizo.

“Ukweli ni kuwa vijana wa Kenya wamekosa maadili. Wazazi wamekosa kuwafunza watoto wao maadili mema. Na watoto wengi ambao ni wanariadha hupotoka punde wanapoondoka nyumbani kwao,” akasema Bw Kipchoge.

  • Tags

You can share this post!

KEMSA yatangaza zabuni nyingine ya bidhaa za corona sakata...

Mahakama yakataa kusitisha uchunguzi wa matamshi ya chuki

T L