Rising Starlets wajitia makali kwa mchuano wa kuingia Kombe la Dunia dhidi ya Uganda

Rising Starlets wajitia makali kwa mchuano wa kuingia Kombe la Dunia dhidi ya Uganda

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 ya kinadada maarufu kama Rising Starlets, imeimarisha matayarisho yake kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Uganda itakayochezwa Septemba 25 jijini Nairobi.

Majirani hawa watarudiana Oktoba 8 nchini Uganda.

Kenya ilianza maandalizi yake Septemba 15 kwa zoezi la kuchagua vipaji chipukizi. Zoezi hilo liliongozwa na kocha wa timu ya watu wazima ya kinadada ya Harambee Starlets, Charles Okere. Kocha huyo ana kikosi cha wachezaji 30.

“Tunaanza kampeni yetu ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia la Under-20 dhidi ya Uganda mnamo Jumamosi na tuna ari ya kupata matokeo mazuri yatakayoweka hai ndoto yetu ya kushiriki Kombe la Dunia 2022,” alisema Okere.

“Kiwango hiki ni muhimu kwetu kwa sababu tunapata kufundisha na kukuza kizazi kipya kitakachoingia timu ya watu wazima,” aliongeza.

Crested Cranes ya Uganda imeratibiwa kuwasili jijini Nairobi hapo Septemba 23 asubuhi.

Mshindi kati ya Kenya na Uganda atamenyana na mshindi wa mchuano kati ya Msumbiji na Afrika Kusini katika raundi ya pili.

Kikosi cha Kenya U20:

Makipa – Ursula Nasimiyu (Dagoretti Mix), Valentine Khwaka (Zetech Sparks), Lucy Kisaga (Gitothua Starlets), Edith Auma (Kibera Queens), Sophy Akinyi (Manyatta Ladies);

Mabeki – Veronica Awino (Gaspo Women), Peris Oside (Nakuru Queens), Mercy Masika (Dagoretti Mix), Joyce Andeo (Beijing FC), Eunice Mwangi (Mpesa Foundation), Invioleta Mukoshi (St John’s Kaloleni), Lucy Kahuga (Madira Girls), Martha Simiyu (Falling Waters), Redempta Mercy (Madira Girls);

Viungo – Medina Abubakar (Uweza Soccer), Drailer Salome (Tigers FC), Lydia Akoth (Zetech Sparks), Maximilla Robi (Beijing FC), Milka Awino (Zetech Sparks), Catherine Aringo (Fortune Ladies), Jane Hato (Madira Girls), Lavender Akinyi (Wiyeta Girls), Mildred Kanyisi (Dagoretti Mix);

Washambuliaji – Fasila Adhiambo (Dagoretti Mix), Elizabeth Muteshi (Nangili Girls), Sylvia Makungu (Acakoro), Shirlyne Opisa (Wiyeta Girls), Charity Midewa (Madira Girls), Joy Kinglady (Zetech Sparks), Catherine Kizito (Kolwa Falcons).

You can share this post!

Messi kusalia nje ya kikosi cha PSG kitakachomenyana na...

Simiyu atumai Oluoch, Keyoga watapona kabla ya Edmonton 7s...