Makala

RITTENBERRY: Kampuni za Afrika zionyeshe utu kwa wafanyakazi wakati huu wa corona

April 30th, 2020 3 min read

NA JORDAN RITTENBERRY

HUKU Covid-19 ikienea barani Afrika, ustawi wa biashara na viwanda umeshuka mno, kutokana na sheria za serikali za kuzuia kudhibiti virusi hivi. Ni wazi kwamba janga hili limebadilisha maisha yetu kabisa.

La msingi ni kwamba, wafanyakazi wanatafuta viongozi wao kuwapa habari na msukumo. Idadi ya uaminifu ya Edelman ya 2020 inaonyesha kuwa wafanyakazi huamini mawasiliano kutoka kwa waajiri wao zaidi kuliko kutoka kwa serikali.

Wahojiwa wa uchunguzi pia wanaamini kwamba waajiri wao wanafaa kuwa mstari wa mbele kushughulikia utandavu huu kuliko serikali, na kwamba viongozi wa biashara wanapaswa kuchukua jukumu la mabadiliko badala ya kungoja serikali iwalazimishe.

Huu ni wakati muhimu kwa wakurugenzi watendaji kuonyesha uongozi wao, kwa huruma.

Haishangazi kwamba wafanyikazi wanataka kuelewa athari ambayo Covid-19 itakuwa nayo kwa mashirika yao, kama ajira na mabadiliko gani ya kimuundo yaweza kuwa mbele.

Ili kujenga uaminifu, mawasiliano ya wazi na ya mara kwa mara na wafanyikazi ni muhimu, na waajiri wanapaswa kuwahakikishia kwamba wanaweka afya zao mstari wa mbele.

Kwa kweli, hii inahitaji kuungwa mkono. Kuna kampuni ambazo zinaweza kutekeleza sera za kazi kutoka nyumbani, sambamba na mwongozo wa serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa wengi, hii ni mara ya kwanza na kunaweza kuwa na shida ambazo zitatokea. Kufanikiwa kwa kufanya kazi kwa mbali kutahijitaji wafanyikazi wawe na vifaa vizuri vya kufanya kazi katika mazingira yao mapya, na mistari ya mawasiliano inapaswa kufunguliwa na kutumiwa mara kwa mara.

Zaidi ya mahali pa kazi, kuna matarajio kwamba mashirika na viongozi wanafaa kusaidia jamii. Inatia moyo kuona kwamba mashirika mengi barani Afrika yanakua kwa kuwekeza wakati na rasilimali katika vita dhidi ya Covid-19 na katika juhudi za misaada.

Nchini Afrika Kusini, watendaji wanatarajia sehemu kubwa za mishahara yao na wanaelekeza akiba kwenye mfuko wa misaada wa kitaifa. Hapa Kenya, kampuni 15 za vyombo vya habari zimetoa nafasi ya matangazo kwa Mfuko wa Dharura unaoongozwa na serikali, licha ya kutegemea sana mapato ya matangazo.

Katika bara lote, viwanda vya nguo vina mapato mapya kutokana na kutengeneza barakoa na vitambaa vingine vya matibabu, ili kuwalipa wafanyakazi wao. Kampuni za vinywaji nazo zinatengeneza viyeyushi.

Janga la corna linapoendelea kusambaa, mashirika yanahitaji kuhakikisha kuwa yanawasiliana na kila kikundi cha wadau, badala ya wachache waliochaguliwa.

Kushirikiana mara kwa mara na kwa uwazi na wauzaji, wafanyikazi, wasimamizi, watumiaji na wanahisa, miongoni mwa wadau wengine, ni muhimu.

Kunafaa kuwe na mpangilio wa hali ya kina, ambao utasaidia kuendesha mikakati ya biashara na maamuzi kulingana na matokeo yanayowezekana. Hii pia inaonyesha utayari wa shirika na huongeza imani ya wadau wengine.

Serikali zinafanya zaidi ziwazavyo kudhibiti virusi hivi kwa amri ya kutotoka nje na kusitishwa kwa shughuli za kawaida.

Watu wamehamasishwa kukaa mbali na wenzao na hii inaweza kuathiri ustawi wa kiakili wa wafanyikazi, wakati pia inaongeza majukumu ya wazazi.

Viongozi wa biashara wanahitaji kufahamu changamoto hizi na wanapaswa kuonyesha msaada kwa wafanyikazi wao kila inapowezekana kwa kuonyesha huruma. Mashirika yatakuza uaminifu kati ya wafanyikazi wao na wataboresha sifa zao wenyewe ndani na nje.

Kuna habari nyingi ambazo sio za kuaminika au kupingana ambazo wafanyikazi wanakutana nazo. Katika nyakati kama hizi, wanataka kusikia kutoka kwa waajiri wao, ambao wanawachukulia kama vichungi vya kuaminika kwa habari muhimu na ya ukweli.

Ili kufanya hivyo, mashirika yanahitaji kukuza mipango ya mawasiliano ya ndani na viongozi wanapaswa kuweka nyakati za kuzungumza na waajiriwa wao.

Zaidi ya yote, viongozi wa biashara wanapaswa kuzungumzwa kwa ukweli, kuongoza kwa kujitolea na uwazi – na kuhakikisha kwamba wanapatikana wanapohitajika.

Kuchukua wakati wa kusikiliza wafanyikazi na kujibu wasiwasi wao ndiyo njia bora ya kujenga uaminifu.

Ninaamini kwamba hatua ambazo viongozi wa biashara watachukua katika wiki na miezi ijayo zinaweza kuamua sifa zao kwa miaka ijayo.

Jordan Rittenberry ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Edelman Africa