Michezo

Rodriguez kumvisha kahaba pete ya uchumba

August 20th, 2018 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

NYOTA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Colombia, James Rodriguez amefichua mipango ya kumvisha kichuna Kendra Lust pete ya uchumba kisha kufunga ndoa na mwanamitindo huyo mkongwe mzawa wa Amerika.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, kiini cha Rodriguez kutaka kumfanya Kendra awe wake wa halali ni ugwiji wa kichuna huyo katika sanaa ya kupiga miereka ya chumbani. Licha ya ukongwe kumtambalia Kendra, mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 40 hana kifani katika masuala ya ukahaba na ufundi wa kuwafungulia wanasoka mzinga wake wa asali.

Hatua ya Rodriguez kuanza kutoka kimapenzi na Kendra ambaye jina lake halisi ni Michele Anne Mason inajiri miezi mitatu tu baada ya mwanasoka huyo anayehudumu uwanjani Allianz Arena kwa mkopo kutoka Real Madrid kutemana na mkewe Daniela Ospina aliyedumu naye katika uhusiano wa ndoa kwa miaka sita.

Mapema mwezi jana, Rodriguez, 27, alikiri kuvutiwa na ubora wa maumbile ya maziwa kifuani pa Kendra ambaye alifanya hima na kupakia mtandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na fowadi huyo.

Mbali na kusifia weledi wa Rodriguez katika upigaji kasia kila aliposhuka kisimani mwake Kendra pia alimsihi sogora huyo kuachana kabisa na mwanamitindo maarufu mzawa wa Urusi, Helga Lovekaty, 26. Kwa mujibu wa gazeti la Fox Sports, Cristiano Ronaldo ndiye kuwadi aliyemrai Helga kujipa kwa Rodriguez aliyekinai asali ya Daniela, kipusa ambaye ni dada yake kipa David Ospina ambaye kwa sasa anawadakia Napoli.

Kubwa zaidi ambalo limewaduwaza mashabiki wa Rodriguez ni jinsi alivyomudu kumridhi

sha Kendra chumbani hasa ikizingatiwa ufundi wake katika masuala ya kufyatua filamu za ngono kama vile F*** Me Silly, Miss Tushy na Let’s Bang the Babysitter miongoni mwa nyinginezo 120.

Kabla ya kuanza kutoka kimapenzi na afisa wa polisi aliyempa mtoto mnamo 2012, Ken-

dra alikuwa kahaba wa kuvua nguo katika vilabu vya starehe tangu 2008. Alitumia fedha alizozipata kutokana na ushiriki wake katika filamu hizo kusomea shahada ya uuguzi kati ya 2009 na 2011.

Kiini cha kusambaratika kwa ndoa ya Rodriguez na Daniela ni jicho la nje la mwanasoka huyo ambaye kwa mujibu wa Daniela ‘alionekana kupagawa’ baada ya kuonjeshwa asali katika mzinga wa Helga mwanzoni mwa mwaka huu.

“Ni rasmi kwamba ndoa iliyodumu kwa miaka sita na nusu kati ya Daniela na Rodriguez imevunjika. Ni maamuzi ambayo yalifikiwa na pande zote mbili baada ya wahusika kushauriana kwa mapana na marefu,” ilisema ripoti iliyochapishwa na gazeti la Marca nchini Colombia. Gazeti hilo lilisisitiza kwamba Rodriguez atasalia na jukumu kubwa la kutimiza maslahi yote ya Salome, mtoto ambaye alijaliwa katika uhusiano wake wa kimapenzi na Daniela, 26.