Michezo

Ronaldo anavyompepesa Miss Bum Bum!

March 9th, 2020 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

JAPO Cristiano Ronaldo anahusiana kimapenzi na kipusa Georgina Rodriguez, nyota huyo wa Juventus ameanza kumnyemelea kichuna Erika Canela, mshindi wa zamani wa taji la Miss Bumbum nchini Brazil.

Kwa mujibu wa Canela, Ronaldo amekuwa akimtumia jumbe, video na picha za mahaba kupitia mtandao wa WhatsApp tangu atawazwe malkia wa Miss Bumbum. Taji hilo lilikuwa likishikiliwa na mrembo Suzy Cortez hadi mwishoni mwa mwaka jana.

Suzy, ambaye ni shabiki sugu wa Barcelona, amewahi kukiri kuteswa na mapenzi anayohisi kwa supastaa Lionel Messi na beki Gerard Pique.

“Ronaldo hachoki kabisa kusifia ukubwa na uzuri wa makalio yangu, licha ya kwamba tayari ana mchumba ambaye amekuwa akimsihi amfanye wake wa halali,” akasema Canela kwa kukiri kwamba, sogora huyo alikutana naye jijini Turin mwanzoni mwa juma lililopita.

Ingawa mipango ya awali ilikuwa ni kukutana kisiri nchini Ureno, mbali kabisa na Georgina, Canela alisisitiza kwamba uzito wa hisia katika jumbe za Ronaldo ulimyeyusha haraka kiasi kwamba asingejizuia wala kusubiri kuvaana kimapenzi na fowadi huyo.

Mnamo 2013, Ronaldo alikiri kumwendea kinyume aliyekuwa mpenzi wake, Irina Shayk kwa kutikisa buyu la asali la kidosho Andressa Urach ambaye alitawazwa mshindi wa Miss Bumbum mwaka huo.

“Ilivyo, dalili zote zinaashiria kwamba Ronaldo huvutiwa sana na vichuna walio na makalio makubwa.

Si bure, amepania kutalii takriban visima vyote vya washindi wa Miss Bumbum, tuzo ambayo hutolewa kila mwaka kwa demu mwenye makalio makubwa na ya kupendeza zaidi nchini Brazil,” akasema Urach kwa kufichua kwamba, Ronaldo amewahi pia kuburudishwa kimapenzi na kipusa Ellen Santana, aliyetawazwa malkia wa Miss Bumbum mnamo 2018.

Mwanzoni mwa 2019, Ronaldo alikiri kuteswa hisia na baadhi ya wapenzi wa zamani wakiwemo wanamitindo Alexandra Mendez na Thomas Imogen.

Alexandra alifichua jumbe alizokuwa akitumiwa na Ronaldo aliyekuwa akimtaka sana kimapenzi kabla ya kukutana na Gerogina ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja.

Ronaldo aliyewahi kutuhumiwa kumnajisi Kathryn Mayorga katika mkahawa mmoja jijini Las Vegas mnamo 2009, aliungama kuwa kwa sasa angalikuwa na Alexandra iwapo asingalimpata Georgina.

Akihojiwa na gazeti la The Sun wiki jana, msemaji wa familia ya Ronaldo alidokeza kwamba sogora huyo anajuta zaidi kukatiza ghafla uhusiano wake na Irina ambaye kwa sasa ni mke wa mtu na mama wa mtoto mmoja. Baada ya kutemwa na Ronaldo, Irina alipata hifadhi mpya ya penzi lake moyoni mwa mwigizaji mzawa wa Amerika, Bradley Cooper ambaye kwa pamoja, wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.

Mbali na Jordana Jardel, Merche Romero, Gema Atkinson, Gema Storey, Tyese Cunningham, Nereida Gallardo, Paris Hilton, Lucia Villalon na Kim Kardashian, vichuna wengine waliowahi kumfungulia Ronaldo mizinga yao ya asali ni Karina Ferro, Soraia Chaves, Mia Judaken, Bipasha Basu, Rita Pereira, Luciana Abreu, Amal Saber, Daniella Chavez, Melanie Martins, Alessia Tedeschi, Maja Daarving, Alesia Riabenkova, Nataly Rincon, Nikoleta Lozanova, Daniella Grace, Paula Suarez na Amy Broadbent.