Michezo

RONALDO: Nina wengi mno, ila vichuna hawa wakinipa asali tena, sitakataa

March 18th, 2019 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

LICHA ya kwamba Cristiano Ronaldo anatoka kimapenzi na kipusa Georgina Rodriguez, mwanasoka huyo bado anateswa hisia na wapenzi wa zamani.

Kileleni mwa orodha hiyo ni wanamitindo Alexandra Mendez, Irina Shayk, Thomas Imogen na Andressa Urach.

Mwishoni mwa wiki jana, Alexandra alifichua jumbe alizokuwa akitumiwa na Ronaldo aliyekuwa akimtaka sana kimapenzi kabla ya kukutana na Gerogina ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja.

Katika mojawapo ya jumbe hizo za WhatsApp, Ronaldo aliyekuwa akichezea Real Madrid wakati huo, alikuwa na uhakika wa kulimenya tunda la Alexandra mwishoni mwa kila mechi ambayo ingemshuhudia akifunga bao.

Ronaldo ambaye kwa sasa anavalia jezi za Juventus, aliungama kuwa kwa sasa angalikuwa na Alexandra iwapo asingempata Georgina.

Ronaldo ambaye anapanga kula yamini ya ndoa na Georgina bado anakabiliwa na kesi ya madai ya kumnajisi Kathryn Mayorga katika mkahawa mmoja jijini Las Vegas mnamo 2009.

Miongoni mwa vichuna wanaomhangaisha Ronaldo kimapenzi ni Jordana Jardel, Merche Romero, Gema Atkinson, Gema Storey, Tyese Cunningham, Nereida Gallardo, Paris Hilton, Lucia Villalon, Erika Canela na Kim Kardashian.

Wanawake wengine ambao wamewahi kumburudisha sogora huyo ni Karina Ferro, Soraia Chaves, Mia Judaken, Bipasha Basu, Rita Pereira, Andressa Urach, Luciana Abreu, Amal Saber, Daniella Chavez, Melanie Martins, Alessia Tedeschi, Maja Daarving, Alesia Riabenkova, Nataly Rincon, Nikoleta Lozanova, Daniella Grace, Paula Suarez na Amy Broadbent.

Akihojiwa na gazeti la The Sun, msemaji wa familia ya Ronaldo alisema kwamba sogora huyo anajutia kukatiza ghafla uhusiano wake na Irina na kwa sasa yupo radhi kuwasha upya mwenge wa penzi lake kwa mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu na mama wa mtoto mmoja.

Baada ya kutemwa na Ronaldo, Irina alipata hifadhi mpya ya penzi lake moyoni mwa mwigizaji mzawa wa Amerika, Bradley Cooper ambaye kwa pamoja, wamejaliwa mtoto mmoja wa kike.

“Tangu ajifungue, Irina amekuwa mrembo ajabu! Maziwa yamemjaa vilivyo kifuani na ghuba zake kuwa kubwa. Mabadiliko haya ni kiini cha Ronaldo kuanza kummezea mate kichuna huyo,” ikasema The Sun.

Ungamo la Ronaldo kuhusu jinsi anavyovutika kwa Irina, linajiri wiki chache baada ya vichuna Rhian Sugden na Andressa Urach pia kukiri kutoka kimapenzi na Ronaldo.