Rooney kurudi shule kusomea ukocha baada ya kuondoka Derby County

Rooney kurudi shule kusomea ukocha baada ya kuondoka Derby County

Na MASHIRIKA

WAYNE Rooney amefichua mpango wa kujifunza zaidi ukocha baada ya kuagana na Derby County akiwa bado na mwaka mmoja katika kandarasi yake na kikosi hicho kilichoteremshwa ngazi hadi Ligi ya Daraja ya Pili nchini Uingereza (League One) mwishoni mwa msimu wa 2021-22.

Rooney kwa sasa anajivunia nusu ya mafunzo ya kozi ya ukocha kwa ajili ya kiwango cha Pro License na anapania kuzuru vikosi mbalimbali vya haiba ndani na nje ya bara Ulaya ili kupata tajriba zaidi.

Nyota huyo wa zamani wa Everton, Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, aliondoka Derby County baada ya umiliki wa kikosi hicho kutwaliwa na bwanyenye David Clowes ambaye tayari amenunua uwanja wa Pride Park.

Rooney anashikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kambini mwa Uingereza kwa mabao 53 kutokana na mechi 120 za kimataifa. Alijiunga na Derby County mnamo Januari 2020 akiwa mchezaji baada ya kuvalia jezi za DC United ya Amerika katika Major League Soccer (MLS).

Aliaminiwa kushikilia mikoba ya ukufunzi kambini mwa kikosi hicho mnamo Novemba 2020 na akaajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili na nusu miezi mitatu baadaye.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

West Ham United wamvizia Jesse Lingard kutoka Manchester...

West Ham wasajili kipa matata wa PSG, Alphonse Areola, kwa...

T L