Ruto aahidi kuepuka madeni akiwa rais

Ruto aahidi kuepuka madeni akiwa rais

Na ANTHONY KITIMO

NAIBU Rais William Ruto ameahidi kuunda serikali itakayoepuka madeni akishinda urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza alipokutana na viongozi wa eneo la Pwani kujadili mahitaji yao ya kiuchumi, Dkt Ruto alisema serikali yake itajumuisha Wakenya wa matabaka, jamii na maeneo yote ya nchi.

Naibu Rais alisema mikutano anayoandaa kuhusu uchumi wa kimaeneo itasaidia kutambua shughuli za kiuchumi katika maeneo husika na kuwezesha watu kunufaika kifedha.

“Nina tajriba kuhusu kuendesha serikali ndiposa tunapojiandaa kuunda serikali ijayo, tunabadilisha mazungumzo ili kujadili kitakachoongeza thamani kwa mwananchi wa kawaida na wala si nani anatoka kabila lipi na yupi atashikilia wadhifa fulani,” alisema Dkt Ruto.

Alisema: “Tunachojadili hapa ni kuhusu mfumo ambao utawezesha kila eneo kuimarisha uchumi wao kwa kuwa maeneo hayo manane nchini yana maslahi na mahitaji maalum.”

You can share this post!

CHOCHEO: Usimkaribie tu, mguseguse…

Atletico Madrid wapiga Real Valladolid na kutia kapuni...