Habari Mseto

Ruto aamuru jeshi lisaidie kusaka miili na kusaidia wahanga Mai Mahiu

May 1st, 2024 1 min read

NA MERCY KOSKEI

RAIS William Ruto Jumanne alitembelea eneo la mkasa Maai Maahiu na kuamuru wanajeshi waungane na kikosi cha kuisaka miili ya walioangamizwa na mafuriko.

Rais pia alisema watu wanaoishi eneo hilo, ambalo limeshatambuliwa kuwa hatari, watalazimika kuondoka kuanzia Jumatano, ili kuokoa maisha.

“Watu wote wanaoishi katika maeneo haya watalazimika kuondoka ndani ya saa 48. Haya ni maeneo ya chemchemi, karibu na mabwawa na popote penye uwezekano wa kutokea maporomoko ya ardhi. Serikali imeweka mikakati ya kuwawezesha kuhama. Tutawatafutia makao ya muda wale watakaohitaji usaidizi,” akasema katika shule ya upili ya Ngeya.

Rais aliahidi kuwa serikali itasimamia gharama za hospitalini pamoja na mazishi kwa familia zilizoathiriwa na mkasa huo.