Habari za Kitaifa

Ruto afuta mawaziri wote kufuatia presha ya Gen Z


RAIS William Ruto amevunjilia mbali Baraza lake la Mawaziri kufuatia wiki tatu za maandamano ya vijana wa kizazi cha sasa almaarufu Generation Z.

Akitangaza hatua hiyo Alhamisi, Julai 11, 2024 katika Ikulu ya Nairobi, Kiongozi wa Taifa alisema kwamba imemlazimu kuchukua hatua hiyo, licha ya kwamba mawaziri hao wamefaulu kutekeleza wajibu mkubwa katika kuimarisha uchumi wa taifa pamoja na kuondoa nchi katika hatari ya kusambaratishwa na madeni.

Dkt Ruto hata hivyo alisema waliobakia katika nyadhifa zao ni Naibu Rais Rigathi Gachagua na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi.