Habari Mseto

Ruto akutana na Lee Njiru

August 26th, 2020 1 min read

NA FASUTINE NGILA

Naibu Rais Dkt William Ruto Jumamosi alikutana na aliyeekuwa msaidizi mkuu wa Rais wa zamani Daniel Arap Moi Lee Njiru.

Naibu Rais kwenye ujumbe kwenye mtandao wa Twitter alisema Njiru “ni nguli, afisa wa kuheshimiwa ambaye mchango wake kwa umma ni wa kuiga.”

Ujumbe huo wa Dkt Ruto Alhamisi ulivutia Wakenya wengi walioshangazwa na nia yake baadaya kumsifia Bw Njuri.

Naibu Rais Jumamosi aliweka pichaa yake na  Bw Njiru kwenye mtandao huo, na kuibua hisia kuwa huenda analenga kutumia tajribaya Bw Njiru anapowania urais 2022.

Bw Njiru alikuwa mkurungezi aliyefanya kwa muda mrefu kwenye huduma za habari za Rais  Moi.

Aliendelea ata  baada ya Rais Moi kusthaafu Desemba 2002 mpaka Rais Moi akafariki Februari mwaka huu.