Ruto apata tikiti ya UDA kuwania urais

Ruto apata tikiti ya UDA kuwania urais

Na NDUBI MOTURI

NAIBU Rais William Ruto, ndiye mgombea urais wa chama cha United Democratic Alliance baada ya Baraza Kuu la Kitaifa (NEC) kumhoji na kupata amehitimu.

Baraza hilo lilikuwa limealika wanaomezea tiketi ya urais ya chama hicho kwa mahojiano kukagua ufaafu wao.

Baraza hilo lilikataa maombi ya wawaniaji wawili Bi Tracy Wanjiru, 23 na Orina Nyamwama kwa kutotimiza mahitaji ya kisheria na kanuni za chama.

Kulingana na Mwenyekiti wa bodi ya uchaguzi ya UDA, Bi Wanjiru hakutimiza hitaji la kuwa na digrii naye Bw Orina hakuweza kulipa ada ya uteuzi iliyowekwa na chama.

Kutemwa kwa wawili hao kumemuacha Dkt Ruto mgombeaji urais wa pekee katika muungano wa Kenya Kwanza.

You can share this post!

Nassir aahidi wapinzani kivumbi uchaguzini

Bodaboda sasa wapumua msako ukisimamishwa

T L