Ruto asema mawaziri katika serikali yake watawajibishwa bungeni

Ruto asema mawaziri katika serikali yake watawajibishwa bungeni

NA SAMMY WAWERU

RAIS mteule William Ruto amesema mawaziri katika serikali yake watakuwa wakiwajibikia utendakazi wao mbele ya bunge la kitaifa na seneti.

Dkt Ruto amesema Jumatano, akiingia rasmi ofisini (endapo ushindi wake hautabatilishwa) atashawishi bunge kubadilisha sheria ili mawaziri wawe wakifika bungeni kuelezea utendakazi wao.

Chini ya utawala wa serikali ya Jubilee aliyoiongoza na Rais Uhuru Kenyatta, Ruto akiwa naibu rais, mawaziri walikuwa wakiitwa mbele ya kamati za mabunge (kitaifa na seneti) kujibu maswali wizara wanazoshikilia doa inapotokea.

“Mawaziri watakuwa wakiwajibikia utendakazi wao mbele ya bunge la kitaifa na seneti, waelezee watu inchofanya serikali kupitia wizara watakazoshikilia,” Dkt Ruto akasema.

Endapo ushindi wake hautabatilishwa, akiapishwa rasmi kuingia ofisini atazindua baraza la mawaziri.

“Lazima wawajibikie majukumu yao…Tutarekebisha sheria, wawe wakifika mbele ya mabunge.”

Dkt Ruto alitoa kauli hiyo akihutubu Karen, Nairobi baada ya kukutana na wajumbe wa Kenya Kwanza waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu Agosti 9, 2022.

  • Tags

You can share this post!

Kipa Opiyo akubali mkataba mpya kuchezea Ingwe

Chebukati sasa awataka polisi kuwakamata waliovamia maafisa...

T L