Ruto ataka wabunge wasipoteze muda wakifufua BBI

Ruto ataka wabunge wasipoteze muda wakifufua BBI

Na Leonard Onyango

NAIBU wa Rais William Ruto amewataka wabunge kujadili masuala nyeti yanayoathiri Wakenya badala ya kujaribu kufufua Mswada wa Marekebisho ya Katiba, maarufu kama BBI, uliotupiliwa mbali na mahakama.

Dkt Ruto aliyekuwa akizungumza nyumbani kwake katika eneo la Sugoi, Kaunti ya Uasin Gishu, alipokutana na ujumbe kutoka Kaunti ya Bungoma, alisema wabunge wanaotaka kufufua BBI ili ‘kubuni nyadhifa zaidi kwa ajili ya wanasiasa wanapoteza wakati’.

Kulingana na Dkt Ruto, wabunge wanafaa kushughulikia kwa dharura mswada wa Hazina ya Bima ya Afya (NHIF) kuwezesha Wakenya wengi kunufaika na matibabu nafuu.

“Wabunge waache kupoteza wakati na fedha za Wakenya kujadili jinsi ya kubadili Katiba ili kuwatengenezea wanasiasa nyadhifa serikalini. Badala yake waangazie mambo yanayohusu mamilioni ya Wakenya,” akasema Dkt Ruto.

Naibu wa Rais alionekana kulenga mswada wa mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni unaolenga kubuni wadhifa wa waziri mkuu atakayekuwa na manaibu wawili.

 

You can share this post!

Magavana wanuia kunyonya raia baada ya 2022

Mwaniaji kiti cha ubunge na mkewe watozwa faini kwa...