Ruto atangaza Baraza la Mawaziri, walioteuliwa sharti wapigwe msasa bungeni kabla ya kuanza majukumu yao rasmi

Ruto atangaza Baraza la Mawaziri, walioteuliwa sharti wapigwe msasa bungeni kabla ya kuanza majukumu yao rasmi

NA MWANDISHI WETU

RAIS William Ruto ametangaza Baraza la Mawaziri saa chache baada ya kufanya kikao na Baraza la Mawaziri waliohudumu chini ya utawala wa serikali ya Jubilee iliyoondoka mamlakani Septemba 13, 2022 alipoapishwa kuwa Rais wa Tano.

Kiongozi wa Amani National Congress Musalia Mudavadi ameteuliwa awe Mkuu wa Mawaziri katika serikali ya Ruto. Mudavadi atasaidia Rais na Naibu Rais RigathiĀ  Gachagua kufuatilia shughuli katika wizara za serikali.

1. Waziri wa Usalama wa Ndani – Prof Kithure Kindiki
2. Waziri wa Masuala ya Kigeni – Dkt Alfred Mutua
3. Waziri wa Elimu – Ezekiel Machogu
4. Waziri wa Kawi – Davis Chirchir
5. Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – Rebecca Miano
6. Waziri wa Ulinzi – Aden Duale
7. Waziri wa Utalii – Penina Malonza
8. Waziri wa Afya – Susan Nakumicha Wafula
9. Waziri wa Michezo – Ababu Namwamba
10. Waziri wa Ardhi – Zacharia Mwangi Njeru
11. Waziri wa Leba – Florence Bore
12. Waziri wa Biashara – Moses Kuria
13. Waziri wa Maji – Alice Wahome
14. Waziri wa Mazingira – Roselinda Soipan Tuya
15. Waziri wa Fedha – Profesa Njuguna Ndung’u
16. Waziri wa Habari na Mawasiliano – Eliud Owalo
17. Waziri wa Kilimo – Franklin Mithika Linturi
18. Waziri wa Huduma za Umma, Jinsia na Usawazishaji – Aisha Jumwa
19. Waziri wa Barabara – Kipchumba Murkomen
20. Waziri wa Sekta ya Biashara Ndogo na za Wastani (SMEs) – Simon Chelugui
21. Waziri wa Uchimbaji Madini – Salim Mvurya
22. Mshauri wa Shirika la Masuala ya Wanawake – Harriet Chigai
23. Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Ndani – Monica Juma
24. Mwanasheria Mkuu – Justin Muturi
25. Katibu katika Baraza la Mawaziri – Mercy Wanjau

Ni lazima mawaziri wapya wapigwe msasa bungeni kabla ya kuapishwa rasmi kuanza kutekeleza majukumu yao endapo watakuwa wameidhinishwa.

  • Tags

You can share this post!

Wakulima walilia serikali gharama ikizidi kupanda

Maafisa watano wa polisi washtakiwa kwa kumuua mahabusu

T L