Ruto ateua Koome kurithi Mutyambai, Kinoti ajiuzulu DCI

Ruto ateua Koome kurithi Mutyambai, Kinoti ajiuzulu DCI

MARY WANGARI

RAIS William Ruto jana Jumanne alimteua Japhet Koome kuwa Inspekta Jenerali mpya wa polisi kuchukua nafasi ya Hilary Mutyambai.

Kulingana na Rais Ruto, hatua hiyo ni kufuatia ombi la kujiuzulu la Hilary Mutyambai kutokana na kile alichosema ni matatizo ya kiafya.

Sasa jina la Bw Koome litapelekwa bungeni ili kupigwa msasa na kuidhinishwa.

Bw Mutyambai hajakuwa kazini tangu mwezi Agosti kwa kile kilichosemekana kuwa matatizo ya kiafya.

Wadhifa wake umekuwa ukishikiliwa na Noor Gabow, ambaye alikuwa akipigiwa upatu kuteuliwa kuchukua mahali pa Mutyambai.

Bw Mutyambai alikuwa amebakisha miezi sita kustaafu.

Rais pia alitangaza kujiuzulu kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI), George Kinoti, na kusema Idara ya Huduma za Polisi itamteua mrithi wake karibuni.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mrengo wa Kenya Kwanza wake Rais Ruto ulimlaumu Bw Mutyambai kwa kile ulichosema ni kukubali polisi kutumiwa kisiasa.

Bw Kinoti naye alilaumiwa kwa madai ya kutumiwa na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta kuwahangaisha waliokuwa wakimuunga mkono.

  • Tags

You can share this post!

IEBC kuandaa kura mpya maeneo kadhaa

Wanasiasa wavuna baraza la mawaziri

T L