Ruto ateua Mwathethe kusimamia KEFRI

Ruto ateua Mwathethe kusimamia KEFRI

NA NICHOLAS KOMU

RAIS William Ruto amemteua mkuu wa zamani wa vikosi vya ulinzi, Samson Mwathethe(pichani), kuwa mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu nchini (KEFRI).

Jenerali (Mstaafu) Samson Mwathethe, amechukua nafasi ya Dkt John Waithaka ambaye aliteuliwa na rais wa zamani Uhuru Kenyatta.

Jenerali huyo atahudumu kwa miaka mitatu.

Vile vile, Rais Ruto amefuta uteuzi wa Agnes Odhiambo kama mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) na kumteua Aden Noor Ali kuchukua nafasi hiyo.

Naye Dkt Jane Lagat ameteuliwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Mfuko wa biashara ya Wanawake kwa kipindi cha miaka mitatu.

Katika Kamati ya Ushauri ya Mashirika ya Serikali, rais aliwateua Joseph Kimani Machiri, Claire Sifuna Wanyama, Ahmed Abdi Rashid, Mary Murangi Mugo, Caroline Cherono Kilisha kuwa wanachama wa kamati hiyo.

Naye Mzee Mwinyi Mzee ameteuliwa kama mwenyekiti wa bodi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Pwani.

Wanachama wa bodi hiyo Muad Mohammed Khalif, Fouzia Abass, Hassan Rashid Nzinga, Jeff Saye, Julius Kariuki Ndegwa, Ibrahim Khamis na Abdullahi Mohamed Abdi pia wameondolewa.

  • Tags

You can share this post!

Chelsea na Fulham watoshana nguvu kwa sare tasa katika...

Everton wapiga Arsenal breki kali katika EPL

T L