Habari Mseto

Ruto kutua Kisii Ijumaa

October 7th, 2020 1 min read

NA JOSEPH WANGUI

Naibu Rais William Ruto anatarajiwa kurudi Kaunti ya Kisii wiki hii kwenye shunguli za kutafuta kura hata baada ya ziara ya awali kuzua vita.

Dkt Ruto anatarajiwa kuzuru maeneo ya Kenyenya, kaunti ya Kisii Ijumaa lakini kwanza atatembelea Kebirigo na Sironga kaunti ya  Nyamira, Alhamisi.

Matembezi yake yake yanakuja huku kaunti hiyo ikijitayarisha kuandaa sherehe za Mashujaa mwaka huu.

Maafisa wakuu serikalini wakiwemo mawwaziri wamekuwa wakizuru kaunti hiyo kuchunguza miradi tofauti kabla ya kuzinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta..

Wataalamu wa siasa wanasema kwamba ziara ya Naibu Rais inalenga kuingia Ikulu 2022.

Dkt William Ruto amekuwa na damu mbaya na Dkt Fred Matiangi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kumteua Matiangi kuchunguza miradi  kazi ambayo ilikuwa kitambo ikifanya na naibu Rais.

Naibu gavana wa Kisii alisema kwamba matembezi ya naibu Rais yalikuwa niyamaana kwa jamii hiyo ya Kisii.

“Atakuwa hapa kwa Harambee na tunaomba vurugu zilizoshuhudiwa wakati alitembea Kisii zisishuudiwe  tena,” alisema akiongeza kwamba wanania ya kubandilisha Maisha ya wanawake kupitia mchango huyo wa pesa.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA