Ruto na Raila wafuatana unyounyo kwenye matokeo ya urais

Ruto na Raila wafuatana unyounyo kwenye matokeo ya urais

NA JUMA NAMLOLA

WAGOMBEA urais William Ruto (UDA) na Raila Odinga (Azimio) jana walifuatana unyonyo kwenye matokeo ya urais yaliyokuwa yakieendelea kujumlishwa.

Vyombo vya habari vilivyokusanya matokeo hayo kutoka kwa tovuti ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), vuluinyesha Bw Odinga na Dkt Ruto wakipishana mara kwa mara.

Tukienda mitamboni, Dkt Ruto na Bw Odinga walikuwa wameachana na chini ya kura 8,000 baada ya kura milioni tano kujumuishwa.

Kulingana na mwenyekiti wa IRBC, Bw Wafula Chebukati, zaidi ya wapigakura 14 milioni waalishiriki kwenye zoezi la Jumanne.

Jana Jumatano Bw Chebukati alisema atatangaza mshindi wa urais punde atakapokusanya fomu zote 46,232 zilizo mikononi mwa wasimamizi wa uchaguzi.

“Sheria inanipa siku saba lakini nitaharakisha shughuli. Uamuzi wa mahakama ya Juu mwaka 2017 ulikuwa wazi kwamba siwezi kutangaza matokeo na fomu zilizotumwa kwa simu. Sitaki uchaguzi ufutwe tena,” akasema Bw Chebukati.

Kufikia Jumatano, hakuwa amepokea hata karatasi moja ya fomu 34A, hata baada ya nakala za picha za fomu hizo kuwa kwenye mtandao wa IEBC.

Mbali na sheria za Uchaguzi kuhimiza kuwepo uwazi, mwaka 2017 Mahakama ya Juu ilifutilia mbali ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta kutokana na dosari za upeperushaji matokeo.

Majaji wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, waliikosoa IEBC kwa kutumia matokeo yaliyotumwa kwa simu, bila kuyathibitisha kutumia nakala zilizokusanywa kwenye vituo vya kupigia kura.

  • Tags

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Dhana ‘iko’ kwa maana ya ‘una’, mna,...

Stephen Mule ahifadhi kiti cha eneobunge la Matungulu

T L