Habari za Kitaifa

Ruto: Nilichagua Gachagua licha ya kupendekezewa kijana mdogo

June 9th, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

RAIS William Ruto amesema ataendelea kufanya kazi na naibu wake Rigathi Gachagua licha ya migogoro inayoendelea ndani ya chama tawala cha UDA.

Akizungumza wakati wa kongamano la kitaifa la maombi la Akorino mjini Nakuru, Rais alionekana kutajia malumbano ambayo yamekuwa yakiripotiwa ndani ya chama chake ambayo yameonekana kumweka Bw Gachagua upande mmoja na wakosoaji wake ambao ni wandani wa Dkt Ruto katika upande wa pili.

“Sisi viongozi wote tafadhali tuheshimiane. Tulifika hapa kwa maombi. Tusitenganishwe tena. Naona mnapata wasiwasi kidogo, msiwe na wasiwasi,” akasema Bw Ruto.

Alikariri kwamba jukumu lake na naibu wake ni kukuza viongozi wachanga kusaidia Kenya kusonga mbele.

“Tusiseme maneno ambayo hayana maana na yanayogawanya watu.”

Kwa upande wake Bw Gachagua alishikilia kwamba kutaka jamii iungane mashinani sio jambo baya huku akitoa mfano wa jinsi walikuwa kwenye hafla ya Akorino ambao pia kama wao wanafaa waungane kama dhehebu kabla ya kuunganishwa na madhehebu mengine na kuwa kanisa.

“Watu wasilete mambo mengine ambayo hayapo. Kuungana ni kuanzia chini kwenda juu, yaani ‘bottom up’. Bw Rais, umoja ambao tunahubiri ni wa Kenya lakini mimi nafanya bottom-up. Mimi nahubiri Amani. Jukumu langu ni kukusaidia Rais kuunganisha taifa,” akasema.