Ruweida aweka historia akichukua kiti cha ubunge

Ruweida aweka historia akichukua kiti cha ubunge

NA KALUME KAZUNGU

MBUNGE Mwakilishi wa Kike wa Lamu, Bi Ruweida Mohamed Obo, ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushinda ubunge Lamu Mashariki tangu 1966.

Bi Obo (Jubilee) alipata kura 5,498 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Bw Ali Athman Sharif (UDA) ambaye ndiye mbunge anayeondoka.

Bw Sharif alipata kura 4,633 kwenye matokeo yaliyotangazwa na afisa wa IEBC wa Lamu Mashariki, Bw Stephen Karani.

Kiti hicho kilivutia wagombeaji wanne.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya kusubiri zaidi kabla kumjua rais mpya

Winga wa kupanda na kushuka Paul Were sasa mali ya Rayon...

T L