LISHE: Sababu kwanini unatakiwa kula matunda mengi kila asubuhi

LISHE: Sababu kwanini unatakiwa kula matunda mengi kila asubuhi

NA MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

KULA matunda kama kiamsha kinywa kutakuchangamsha, kutakusaidia katika kupoteza uzito na kuchochea njia yako ya utumbo.

Zaidi ya hayo, kiamsha kinywa chepesi na safi ni njia bora ya kutoka kwa masaa uliyofunga hadi wakati wa kula. Milo nzito kama soseji, bekoni na mayai huzuia mafuta kusiagika kwa siku nzima.

Chaguo kama hizo za kiamsha kinywa zitahisi nzito ndani ya matumbo yetu na huleta hisia za uchovu siku nzima. Kubadili kutumia matunda kutaleta maboresho makubwa kwa afya yako.

Mwili wako hupitia kipindi kikali zaidi cha kuondoa sumu masaa ya asubuhi. Matunda yatatoa nishati zaidi kwa mchakato huu ikilinganishwa na vyakula vya kupambana na kuondoa sumu vyenye mafuta mengi.

Huimarisha mchakato wa kimetaboliki

Kula matunda ndio njia bora ya kuanza siku yako kwani ni rahisi kwa mwili wako kusaga kitu cha kwanza asubuhi. Pia husababisha kuongezeka kwa viwango vya kimetaboliki kwa saa chache zijazo shukrani kwa utitiri wa sukari ya asili ya matunda.

Kuchochea njia yako ya utumbo

Matunda kwa kiamsha kinywa husaidia kwa kutoa vimeng’enya muhimu, nyuzinyuzi na viuatilifu ili kuchochea juisi ya usagaji chakula tumboni mwetu na kuosha taka za zamani kutoka siku iliyotangulia. Nyuzinyuzi za matunda husafisha koloni vizuri na kukuacha uhisi mwepesi na umeburudishwa kwa siku nzima.

Kuamsha mwili wako

Mwili wako unahitaji sukari asilia ya matunda mara tu unapoamka. Jaribu kubadilisha unywaji wa kahawa na kikombe cha shurubati ya matanda asili kwa kutafanya ubongo wako uwe mwepesi na uchangamfu.

Kupoteza uzito

Matunda hukupa lishe bora na husaidia kuondoa sumu nyingi kutoka kwa matumbo yetu. Kula matunda siku nzima kuanzia asubuhi kutaondoa sumu na kusafisha mfumo wako, na hivyo kusababisha kupoteza uzito. Dhana potofu ya kawaida ni kwamba kula kiamsha kinywa kilichojazwa na protini ya wanyama kutakuzuia kula sana kwa siku. Walakini, kula zaidi asubuhi kunaweza kusababisha kula zaidi baadaye mchana, na kusababisha kupata uzito.

Kuimarisha mfumo wetu wa kinga

Kwa kunywa smoothie yenye afya dhidi ya bekoni na soseji itakuwa bora zaidi kwa mfumo wako wa kinga na afya kwa ujumla kwa muda mrefu. Matunda yana kiasi kikubwa cha vitamini na vioksidishaji, ambayo husaidia kuimarisha mfumo wetu wa kinga na kuzuia magonjwa ya kuambukiza.

Inatengeneza mazingira ya alkali katika mwili wetu

Watu wengi wanafikiri kwamba matunda yana asidi nyingi. Kwa kweli, limau ni moja ya matunda yenye alkali zaidi duniani. Ingawa inaweza kuwa na asidi kwa asili, mara tu yanapofika tumboni, madini hutengana, na kuifanya kuwa ya alkali. Kimsingi, matunda yote ni ya alkali, hivyo ni vizuri kula kila asubuhi.

Kupunguza uvimbe wa tumbo

Nyuzi za matunda zitaondoa uchafu wa zamani kwenye mfumo wako wa usagaji chakula na kuondoa uvimbe wa sehemu ya chini ya tumbo. Matunda yenye maji mengi kama tikiti maji hufanya kama diuretiki asilia ya kuondoa sodiamu yoyote ya ziada.

Tikitimaji. PICHA | MARGARET MAINA

Ni muhimu kudumisha lishe yenye afya na uwiano, wakati inamaanisha kubadili matunda, kumbuka kujumuisha mboga nyingi na nyama isiyo na mafuta ili kupata ulaji wa kutosha wa virutubisho.

  • Tags

You can share this post!

Fahamu ni kwa nini unashauriwa kunywa maji mengi

Shule ya msingi ya Jamhuri, Thika kugeuzwa iwe ya upili

T L