Safari ya mwaniaji mwenza wa Ruto tangu kijijini Hiriga

Safari ya mwaniaji mwenza wa Ruto tangu kijijini Hiriga

NA STEPHEN MUNYIRI

MWANIAJI mwenza wa urais wa muungano wa Kenya Kwanza, Rigathi Gachagua alizaliwa mnamo 1965 katika kijiji cha Hiriga, Kata ya Ruguru iliyoko eneobunge la Mathira, Kaunti ya Nyeri.

Alisomea katika Shule ya Msingi ya Kabiru-ini kati ya 1971 na 1977.

Baadaye, alielekea katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Kianyaga katika Kaunti ya Kirinyaga kati ya 1978 na 1981, alikofanya mtihani wa shule ya upili mnamo 1983.

Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi alikosomea Shahada ya Fasihi na Utawala kati ya 1985 na 1988.

Kati ya 1988 na 1989, alihudumu kama msaidizi wa kibinafsi wa aliyekuwa mbunge wa Mathira wakati huo, Davidson Ngibuini Kuguru.

Katika miaka ya tisini, Bw Gachagua alihudumu kama mkuu wa taarafa (DO) katika maeneo kadhaa nchini.

Baadaye, alihudumu kama msaidizi wa kibinafsi wa aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma wakati wa utawala wa marehemu Daniel Moi, Prof Philip Mbithi kati ya 1990 na 1992.

Bw Gachagua pia alihudumu kama msaidizi wa kibinafsi wa Rais Uhuru Kenyatta kati ya mwaka 2002 na 2006.

Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Mathira kwenye uchaguzi wa 2017 kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

  • Tags

You can share this post!

Yaibuka naibu rais alikuwa amefanya uamuzi wa mbunge wa...

Kindiki sasa aamua kujiondoa katika siasa baada ya uchaguzi...

T L