Habari

Safaricom yamteua Michael Joseph kaimu Afisa Mkuu Mtendaji

July 2nd, 2019 1 min read

Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Safaricom imemteua Afisa Mkuu Mtendaji wa zamani Michael Joseph katika wadhifa huo kuhudumu kama kaimu baada ya kifo cha Bob Collymore kilichotokea Jumatatu, Julai 1, 2019.

Kwenye mkutano maalumu wa wakurugenzi Jumatatu, bodi ya kampuni iliamua kumteua Michael Joseph kuongoza ambapo utekelezaji unaanza mara moja.

“Bw Joseph atashikilia wadhifa huo hadi pale kampuni itatoa tangazo kuhusu uteuzi wa kudumu,” Safaricom ilisema kwenye taarifa.

Bw Joseph ni mwanachama katika bodi ya Safaricom na ni mwenyekiti wa sasa wa Kenya Airways.

Collymore alichukua wadhifa huo kutoka kwa Bw Joseph mnamo Novemba 2010.