Safaricom yazidi kupaa

Safaricom yazidi kupaa

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imeendelea kutamba baada ya kupata ongezeko la faida la asilimia 20.22 kwa miezi sita kufikia Septemba 2018.

Ongezeko hilo linahusishwa ongezeko la biashara ya M-Pesa.

Ripoti hii ni kulingana na kampuni hiyo katika ripoti Ijumaa. Baada ya kutozwa ushuru, Safaricom iliripoti faida ya Sh31.5 bilioni ikilinganishwa na Sh26.20 bilioni mwa mmoja uliopita.

Kampuni hiyo ya mawasiliano ambayo hisa zake katika soko la hisa la Nairobi zilizaa Sh35.52 kutoka M-Pesa, ongezeko la asilimia 18 kutoka Sh30.05 bilioni mwaka mmoja uliopita.

Ukuaji wa matumizi ya data yalipungua katika kipindi hicho, ambapo watumiaji katika kipindi hicho waliipa kampuni hiyo Sh19.45 bilioni.

Mapato kutokana na kupiga simu yaliongezeka asilimia 1.4, hadi Sh48.03 bilioni.

Lakini mapato kutokana na kutuma ujumbe hayakuongezeka kwa kiasi kikubwa – asilimia 1.2 pekee, kufikia Sh8.82 bilioni.

You can share this post!

#GoogleWalkOut: Wafanyakazi wagoma kulalamikia dhuluma za...

Kenya yaikokosoa Uchina kuondoa marufuku ya biashara ya...

adminleo