Safina yamtaka Jimi atafute urais kupitia tiketi yake

Safina yamtaka Jimi atafute urais kupitia tiketi yake

NA WINNIE ONYANDO

CHAMA cha Safina jana Jumapili kilimpendekeza Jimi Wanjigi apeperushe bendera ya urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Mwenyekiti wa chama hicho, Duncan Nyale alisema kuwa wengi wametuma ombi la kuungana na chama hicho ila wangependa bwanyenye Wanjigi awanie kiti cha urais kupitia chama chao.

“Sisi kama chama, tungependa Bw Wanjigi apeperushe bendera ya urais kupitia chama chetu,” akasema Bw Nyale.

Kwa upande mwingine, Bw Nyale alisema kuwa chama chao hakiko tayari kujiunga na muungano wowote wa kisiasa.Alisema kuwa wako tayari tu kushirikiana na vyama vingine ili kuunda serikali.

“Hatutajiunga na muungano wowote wa kisiasa. Atakayepeperusha bendera ya urais kupitia chama cha Safina ataendeleza kampeni zake hadi siku ya kupiga kura,” akasema Bw Nyale.

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Wito wa Rais Kenyatta kaunti zilipe...

Ngirici kuwania ugavana kama mwaniaji huru

T L