Habari za Kitaifa

Sajini Mkuu John Kinyua alikuwa akutane na familia akitoka ziara ya kikazi Bonde la Ufa

April 19th, 2024 1 min read

Na GEORGE MUNENE

FAMILIA ya Sajini Mkuu John Kinyua Mureithi aliyeangamia baada ya helikopta ya kijeshi kuanguka Alhamisi, ameacha familia changa na alikuwa tegemeo la wazazi wake.

Familia ilisema mwanajeshi huyo alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa familia jana baada ya kutoka ziara ya kikazi kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Jamaa wa mwanajeshi fundi wa mitambo John Kinyua Mureithi akijawa na majonzi kufuatia habari za kifo chake kufuatia ajali ya ndege Elgeyo Marakwet. Picha|George Munene

Tayari familia hiyo imeanza maandalizi ya mazishi ya Bw Kinyua, 38, aliyekuwa miongoni mwa wanajeshi kumi, akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Francis Ogolla waliohusika kwenye ajali hiyo ya helikopta wakiwa kazini.

Kulingana na familia ya marehemu walifahamu kifo cha mpendwa wao kwa mshtuko mkubwa.

Familia hiyo ilisema ilizungumza na Bw Kinyua kwa simu Alhamisi na kupanga mkutano wa familia ambao ulipangwa kufanyika Jumamosi.