Sakaja aisihi serikali kukumbuka Nairobi katika ugavi wa mgao wa kilimo

Sakaja aisihi serikali kukumbuka Nairobi katika ugavi wa mgao wa kilimo

NA SAMMY WAWERU

GAVANA wa Nairobi Johnson Sakaja ameiomba serikali kuu kukumbuka kaunti yake kwenye ugavi wa mgao kwa sekta ya kilimo.

Bw Sakaja amesema Nairobi ni mojawapo ya kaunti zinazoendeleza kilimo cha kisasa.

Alitaja mfumo wa mvungulio (greenhouse), ufugaji wa kuku na mbuzi kama miongoni mwa shughuli ya kilimo-ufugajibiashara inayofanyika viungani mwa jiji la Nairobi.

“Tuna baadhi ya wakazi wenye nafasi za ardhi wanaokuza mimea inayochukua muda mfupi kuzalisha. Hivyo basi tunasihi serikali kutukumbuka kwenye mgao wake wa kilimo kwa kaunti,” Gavana huyo akaomba.

Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2022/2023 hata hivyo yalisomwa Aprili na Waziri wa Fedha na Hazina ya Kitaifa anaayeondoka, Ukur Yatani.

Sekta ya kilimo ilitengewa mgao wa Sh63.9 bilioni.

Chini ya Katiba ya sasa iliyozinduliwa 2010 na kuanza kutumika 2013, sekta ya kilimo imegatuliwa.

  • Tags

You can share this post!

Waluke atorokea bungeni yeye na Wakhungu wakirudishwa jela...

Mhariri wa KBC Millicent Owuor kujua hatima yake Oktoba 11

T L