Habari za Kitaifa

Sakaja amtaka Gachagua ‘aache vita na Rais’

May 29th, 2024 1 min read

NA KEVIN CHERUIYOT

GAVANA wa Nairobi Johnson Sakaja amemtaka Naibu Rais Rigathi Gachagua kukoma ‘kuzua vita’ na mkubwa wake, Rais William Ruto.

Akizungumza Jumatano katika Ukumbi wa Bomas wakati alipokutana na wajumbe wa UDA wanaounga mkono azma yake ya kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Tawi la Nairobi, Gavana huyo alimtaka Bw Gachagua kumheshimu Rais na viongozi wengine waliochaguliwa.

Bw Sakaja alisema ameshangaa kumuona Naibu Rais akilalamika kwamba ametengwa serikalini, “ilhali alikuwa akitetemesha viongozi wengine katika siku zilizopita.”

“Nimepitia mengi, na si rahisi kunitishia. Hakuna aliye na haki ya kusema kwamba nilipewa kiti. Nilichaguliwa,” akasema Bw Sakaja.

“Huwezi kunyanyasa watu kwa miaka miwili, halafu ukitajwa kwa wiki moja unaanza kulia.”