HabariSiasa

SAKATA YA NYS: Orodha ya washukiwa waliokamatwa Jumatatu

May 28th, 2018 1 min read

FAUSTINE NGILA na STELLA CHERONO 

MAAFISA wa upelelezi Jumatatu asubuhi wamekuwa mbioni kuwakata washukiwa washukiwa wakuu wa wizi wa mabilioni ya Shirika la Huduma ya Vijana (NYS).

Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai (pichani kushoto) alitiwa pingu huku maafisa wa upelelezi wakiapa kuwakamata watu wengine 48 wanaoshukiwa kumeza mabilioni kwa kufanya kazi hewa.

Bw Ndubai alikamata jijini Nairobi pamoja na wengine 12 ambao wanazuiliwa katika vituo vya polisi vya Central, Muthaiga na Gigiri wakisubiri matayarisho ya mashtaka na kufikiwa mahakamani.

Haya yalithibitishwa na Afisa Mkuu wa Upelelezi katika Kaunti ya Nairobi, Ireri Kamwande.

Watu wengine wannewa familia ya Ngirita wamethibitishwa kukamatwa mjini Naivasha kuhusiana na sakata hiyo.

Wanne hao ni Ann Wambere Ngirita, aliyepokea Sh59 milioni kwa ‘kuuza hewa’, Gicini Ngirita (kakaye), Phyllis Ngirita (dadaye) na mama yao Lucy Wambui Ngirita.

Orodha ya washukiwa waliokamatwa kufikia sasa

 • Bi Lillian Mbogo Omollo, Katibu wa Huduma kwa Umma (alijiwasilisha kwa polisi)
 • Bw Richard Dubai, Mkurugenzi Mkuu wa NYS
 • Bw Sam Muchuki
 • Bw Peter Muchui
 • Bw Matano Odoyo, NYS
 • Bw James Thuita Nderitu, mfanyabiashara
 • Bi Yvonne Wanjiku Ngugi, mfanyabiashara
 • Bw Sammy Mbugua
 • Bw Timothy Kiplangat Rotich
 • Bw Wellanalo Mulupi, NYS
 • Bw David Kirui
 • Bw Ferdinard Matavo
 • Bi Keziah Mwangi, NYS
 • Bw Duba Galgalo
 • Bw Isaiah Adalo Chopia
 • Bi Ann Wambere Wanjiku Ngirita (aliyeuzia NYS hewa)
 • Bi Lucy Wambui Ngirita, mamaye Wambere
 • Bi Phyllis Ngirita, dadaye Wambere
 • Bw Gicini Ngirita, kakaye Wambere

Hii ni baada ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) inayosimwamiwa na Bw George Kinoti kukamilisha sehemu ya uchunguzi wake na kuwasilisha faili 10 za upelelezi kwa afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) inyoongozwa na Bw Noordin Haji (pichani kulia), usiku wa kuamkia Jumapili.

Upelelezi umekuwa ukilenga kampuni na watu binafsi wapatao 40 wakiwemo maafisa wakuu serikalini wanaoaminika kuhusika katika ufujaji wa karibu Sh9 bilioni za NYS.