Michezo

Salah kuongoza mashambulizi ya Misri Kombe la Dunia licha ya kujeruhiwa na Ramos

May 28th, 2018 2 min read

Na MASHIRIKA

STRAIKA matata wa Liverpool na Misri Mohamed Salah jana aliwaondolea mashabiki wake hofu kuwa huenda jeraha alilopata katika fainali ya Klabu Bingwa Uropa likamzuia kutetemesha nyavu kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi linaloanza Download Guide to bodybuilding movements PDF 2021 letromina bodybuilding room in agen, jean baptiste de baudre high school – (lot-et-garonne). hapo Juni 14.

Salah alisema yuko tayari kuongoza mashambulizi ya Misri kwenye kipute hicho, licha ya kupata jeraha la begani alipokabiliwa na difenda wa Real Madrid, Sergio Ramos jijini Kiev, Ukraine.

Salah, 25, alitoka uwanjani huku machozi yakimbubujika katika dakika ya 30 na kuwaacha mashabiki kwa hofu kuu kuwa huenda jereha hilo likamuondoa kwa orodha ya wachezaji wa Misri kwenye Kombe la Dunia.

“Mapenzi na uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki ndio nahitaji kunipa nguvu kuwika Urusi,” akasema Salah.

Misri itaingia uwanjani Juni 15 kuchuana na Uruguay katika uwanja wa Yekaterinburg.

Baada ya mechi hiyo ya Kiev, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema jeraha hilo ‘ni baya sana, na halikuonekana kupona hivi karibuni.

Lakini shirika la soka nchini Misri lilitoa taarifa likisema kuwa uchunguzi wa X-rei ulionyesha Salah alikuwa na uvimbe kwenye bega kutoka na jeraha na kuwa atapona haraka na kusafiri Urusi.

Mshambuliaji huyo ambaye amefuma mabao 44 msimu huu, alijaribu kuendelea na mechi baada ya kuangushwa na Ramos dakika ya 26, lakini hakuweza kuvumilia uchungu aliohisi na kulazimika kuondolewa na nafasi yake ikajazwa na Adam Lallana.

Misri almaarufu ‘The Pharaohs’ wanatawaliwa na hamasa ya kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu 1990.

Ingawa hivyo, wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kuwazidi maarifa Uruguay ambao ni mabingwa mara mbili wa Kombe la Dunia ugani Central, Yekaterinburg.

Vijana hao wa kocha Hector Cuper watajaribu kuilaza Urusi katika mchuano wao wa pili wa Kundi A mnamo Juni 19 ugani Krestovsky kabla ya kufunga rasmi kampeni za makundi dhidi ya Saudi Arabia mnamo Juni 25 uwanjani Volgograd.

Misri kwa sasa wanaorodheshwa na FIFA katika nafasi ya 31 duniani na wajitosa katika Kombe la Dunia wakijivunia motisha ya kutinga fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) 2016 ila wakazidiwa maarifa na Indomitable Lions kutoka Cameroon.

Kikosi cha Misri ambacho kinashiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya tatu katika historia ndicho kinachojivunia mataji mengi zaidi ya AFCON barani Afrika.

Katika safari yao ya kuelekea Urusi mwaka huu, Misri waliwabwaga Uganda, Ghana na Jamhuri ya Congo huku wakifunga jumla ya mabao manane pekee kutokana na mechi sita.

Urusi watakaopania kuchuma nafuu kutokana na wingi wa mashabiki wao wa nyumbani wanatazamiwa kuibuka kileleni mwa Kundi A huku Saudi Arabia wakipigiwa upatu wa kukokota nanga mkiani.

Hivyo, kibarua kizito zaidi kwa Misri ni jinsi ya kuwapiku Uruguay ambao kwa sasa wanajivunia safu bora zaidi ya uvamizi duniani.

Mashambulizi ya Uruguay yatanogeshwa zaidi na weledi wa nyota Edinson Cavani (PSG) na Luis Suarez (Barcelona).

Hata hivyo, Misri ambao hawajawahi kusajili ushindi wowote kwenye fainali za Kombe la Dunia, watapania sana kutegemea ushirikiano kati ya Salah na kiungo wa Arsenal, Mohamed Elneny.

Masogora wengine wanaotazamiwa kutamba zaidi ndani ya jezi za timu ya taifa ya Misri ni Omar Gaber na Ramadan Sobhi aliyesajiliwa na Stoke City mnamo 2016 baada ya kuridhisha sana akiwasakatia Al Ahly.