Samaki waoza kwa ukosefu wa jokofu la hifadhi

Samaki waoza kwa ukosefu wa jokofu la hifadhi

Na KALUME KAZUNGU

WAVUVI katika Kaunti ya Lamu, wamelalamikia ukosefu wa vyombo vya kuhifadhi samaki wakisema imewaletea hasara tele.

Kulingana nao, idadi kubwa ya samaki wanaovuliwa kila siku huoza kabla soko lipatikane.Wameomba serikali ya kaunti, kitaifa na wahisani kuwanunulia majokofu ili kuwaepusha na hasara wanazopata.Mwenyekiti wa Muungano wa Wavuvi (BMU) kwenye kisiwa cha Lamu, Bw Abubakar Twalib, alitaja kukosekana kwa miundomisngi ifaayo kwenye sekta ya uvuvi kuwa kizingiti kikuu kinachopelekea sekta hiyo kukosa kupanuka miaka yote.

Bw Omar Malau ambaye ni mvuvi wa kisiwa cha Ndau pia alitaja ukosefu wa soko la pamoja eneo la Lamu kuwa changamoto kubwa inayokabili wavuvi eneo hilo.Wavuvi wa Lamu hutegemea soko la samaki la miji ya Malindi, Kilifi na Mombasa.Bw Malau anasema samaki wengi wamekuwa wakioza wakati wanaposafirishwa mbali.

“Ninaamini hapa Lamu tukiwa na kiwanda cha samaki, soko litakuwepo na tutapunguza hizi,” akasema Bw Malau.Wavuvi hao pia waliirai serikali kusitisha msako unoendelea wa vyavu haramu kwenye bahari ya Lamu, wakisisitiza kuwa msako huo umewasukuma wengi kuacha shughuli zao za uvuvi kwa kuhofia kukamatwa baharini. Lamu ina zaidi ya wavuvi 7,000.

You can share this post!

Ruto, Raila wakoroga chama cha Kingi PAA

Mzee Oroni bado anatimua mbio hafikirii kustaafu licha ya...

T L