Sambakhalu FC watwaa Lwanga Cup

Sambakhalu FC watwaa Lwanga Cup

NA JOHN ASHIHUNDU

SAMBAKHALU FC wameibuka mabingwa wa kombe la Charles Lwanga katika Wadi ya Isukha Kusini, eneo la Shinyalu, Kaunti ya Kakamega.

Mabingwa hao walishinda taji hilo baada ya kuibwaga Mukumu Lyon FC 3-2 kwenye fainali ngumu iliyochezewa Mukumu Boys High School, Jumamosi. Eleven Starlets walitwa ubingwa kwa upande wa akina dada baada ya kuichapa Sambakhalu Ladies FC 2-0.

Kwa ushindi huo, Sambakhalu ambao walifuzu baada ya kuichapa Sigalagala 2-0 kwenye nusu-fainali walikabidhiwa Sh110,000, wakati Mukumu Lyon waliobwaga Shipalo 3-1 kwenye nusu-fainali nyingine wakiondoka na Sh60,000. Shipalo walitandoika Sigalagala 3-0 na kumali katika nafasi ya tatu na kupata Sh30,000.

Eleven Starlets walioibuka mabingwa kwa upande wa wanawake waliondoka na Sh10,000 wakati  Sambakhalu Ladies wakipata Sh5,000 kwa kumaliza katika nafasi ya pili. Shipalo, Banana, Mukumu Queens na Lugango pia zilishiriki katika kiwango hicho.

Diwani wa Isukha Kusini, Charles Lwanga (aliyevalia shati-tao jeupe) na Mwakilishi wa Kike wa Kakamega Elsie Muhanda wawatunuka washindi wakati wa michuano ya Lwanga Cup katika shule ya Mukumu Boys High School. PICHA | HISANI

Lwanga ambaye ndiye MCA Isukha alisema lengo ya mashindano hayo ni kutafuta vijana walio na vipaji ambao wataunda timu ya muunano ya kuwakilisha wodi ya Isukha Kusini ligini msimu ujao.

Mgeni wa heshima, Elsie Muhanda ambaye ni Mwakilishi wa akina mama Kaunti ya Kakamega alisema kuna haja ya viwanja vya mashinani kukarabatiwa kwa lengo la kuimarisha vipawa vya vijana.

  • Tags

You can share this post!

Wasiwasi Urusi ikifanya ushauri na Afrika Kusini

Mkuu wa zamani NHIF aondolewa kesi ya Sh1.1b

T L