Michezo

Sanchez hatarini kutemwa kwa kumezea mwanachuo

February 19th, 2018 1 min read

Na MASHIRIKA

KICHUNA Mayte Rodriguez ambaye amekuwa akitoka kimapenzi na nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez, ametishia kukatiza uhusiano wake na fowadi huyo mzawa wa Chile wiki moja tu baada ya kuungana naye jijini Manchester, Uingereza.

Hii ni baada ya mwanafunzi mmoja jijini London kupasua mbarika kuhusu jinsi ambavyo amekuwa akimfungulia Sanchez mzinga wake wa asali katika uhusiano wa siri uliodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wakati mfumaji huyo alipokuwa akizivalia jezi za Arsenal.

Kwa mujibu wa Paulina Sobierajska, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha London, Sanchez amekuwa na mazoea ya kulidokoa tunda lake mara mbili kwa mwezi kwa Sh300,000.

Alexis Sanchez wa Man United akiwa na kichuna Mayte Rodriguez. Picha/ Hisani

Katika mahojiano yake ya wiki jana na gazeti la The Sun, Paulina, 20 alikiri Sanchez alivutiwa na ukubwa wa makalio na mapaja yake mnamo Januari 2017 baada ya sadfa kuwakutanisha katika mkahawa mmoja wa kifahari jijini London.

“Sadfa ilitukutanisha katika mkahawa wa Mayfair Novikov, London. Haikumchukuwa muda mrefu kabla ya Sanchez kumtuma mmoja wa marafiki waliokuwa wakinywa naye tembo kunieleza jinsi alivyozinguliwa na urembo wangu.”

“Tulianza kuwasiliana kupitia jumbe fupi za simu na punde akaanza kunitumia arafa za kimapenzi huku akisifia ukubwa wa makalio, mapaja na maziwa yangu pamoja na weusi wa nywele zilizoanguka tawili mabegani pangu. Sikusita kujilegeza kwake na kumpa tunda alidokoe apendavyo.

Hata hivyo, uhusiano wa videge hao uliingia mdudu baada ya Paulina kufahamikiwa kwamba Sanchez aliyekuwa akimwahidi ndoa kwa siku nyingi alikuwa pia akiramba vya Mayte.