Sapit: Msiwachague wasiotekeleza ahadi

Sapit: Msiwachague wasiotekeleza ahadi

Na KENYA NEWS AGENCY

KIONGOZI wa Kanisa la Anglikana Nchini Askofu (ACK) Jackson Ole Sapit amewataka wanasiasa ambao wanasaka viti mbalimbali vya uongozi kuoanisha ahadi zao za kampeni kulingana na hali ya sasa ya kiuchumi nchini.

Askofu Sapit alisikitishwa na matamshi ya baadhi ya wanasiasa ambao wanatoa ahadi ambazo hata wao wanafahamu hawawezi kutekeleza wakichaguliwa Agosti 9.

“Yafaa tuwaambie Wakenya ukweli na kutoa ahadi ambazo tutahakikisha zinatekelezwa. Wanasiasa wana wajibu wa kusema ukweli badala ya kutoa ahadi ambazo wanafahamu hawatatekeleza,” akasema Askofu Sapit.

Pia aliwataka wanasiasa wawe vielelezo bora kwa wananchi kwa kudhihirisha uzalendo wao wakati huu kampeni zinaendelea kuchacha.

“Hasa wanasiasa wetu wanafaa wakumbatie mbinu za amani za kusuluhisha mgogoro kati yao badala ya kukumbatia ghasia. Hii ndiyo itaonyesha sifa nzuri kwa Wakenya ambao watawaiga na kujizuia kushiriki maovu,” akaongeza Askofu Sapit.

Pia askofu huyo aliwataka Wakenya wajisajili kama wapigakura kipindi hiki ambapo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Nchini (IEBC) inaendelea kuwasajili wapigakura wapya.

Askofu Sapit yupo kwenye ziara ya wiki moja katika Kaunti ya Kakamega ambako anakutana na viongozi wa dayosisi mbalimbali za kanisa hilo.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Azimio la Muhando

Shirika latilia shaka maandalizi ya IEBC

T L