Habari Mseto

Saratani: Himizo wanaume wapimwe

January 14th, 2024 1 min read

NA JURGEN NAMBEKA

WIZARA ya afya kaunti ya Taita Taveta imewaomba wanaume kaunti hiyo kujitokeza kila mara kupimwa saratani ya tezi dume.

“Serikali imekuwa ikiweka juhudi kuhakikisha kuwa tunabadilisha mtazamo wetu wa kutafuta huduma za afya. Tunawataka wakazi wabadilishe mawazo yao kuhusu kutafuta huduma haswa kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara kuhusiana na saratani ya tezi dume,” akasema Waziri wa afya Bw Gifton Mkaya alipohudhuria mazishi ya mmoja wa wafanyakazi wa wizara ya afya kaunti hiyo.

Kulingana naye, kujua hali ya ugonjwa mapema huenda kukapunguza maafa na kuhakikisha wakazi wanaweza kusimamia afya yao ipaswavyo.